Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 146

1Msifuni Bwana! + 146:1 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah. 1 Ee nafsi yangu, umsifu Bwana, 2

2Nitamsifu Bwana maisha yangu yote; 1 nitamwimbia Mungu wangu sifa 2 wakati wote niishipo. 1

3Usiweke tumaini lako kwa wakuu, 2 kwa wanadamu ambao hufa, 2 ambao hawawezi kuokoa. 1

4Roho yao itokapo hurudi mavumbini, 2 siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma. 1

5Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, 2 ambaye tumaini lake ni katika Bwana, Mungu wake, 1

6Muumba wa mbingu na nchi, 2 na bahari na vyote vilivyomo ndani yake: 1 Bwana anayedumu kuwa mwaminifu 2 milele na milele. 1

7Naye huwapatia haki walioonewa 2 na kuwapa wenye njaa chakula. 1 Bwana huwaweka wafungwa huru, 2

8Bwana huwafumbua vipofu macho, 1 Bwana huwainua waliolemewa na mizigo yao, 2 Bwana huwapenda wenye haki. 1

9Bwana huwalinda wageni 2 na kuwategemeza yatima na wajane, 2 lakini hupinga njia za waovu. 1

10Bwana atamiliki milele, 2 Mungu wako, ee Sayuni, 2 kwa vizazi vyote. 1 Msifuni Bwana.

← Psalms 145Read In The App, Free →Psalms 147 →

Study Psalms 146

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150