Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 66

1Mpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote! 2

2Imbeni utukufu wa jina lake; 2 mpeni sifa zake kwa utukufu! 1

3Mwambieni Mungu, “Jinsi gani yalivyo ya kutisha matendo yako! 2 Uwezo wako ni mkuu mno kiasi kwamba 2 adui wananyenyekea mbele zako. 1

4Dunia yote yakusujudia, 2 wanakuimbia wewe sifa, 2 wanaliimbia sifa jina lako.” 1

5Njooni mwone yale Mungu aliyoyatenda, 2 mambo ya kutisha aliyoyatenda 2 miongoni mwa wanadamu! 1

6Alifanya bahari kuwa nchi kavu, 2 wakapita kati ya maji kwa miguu, 2 njooni, tumshangilie. 1

7Yeye hutawala kwa uwezo wake milele, 2 macho yake huangalia mataifa yote: 2 waasi wasithubutu kujiinua dhidi yake. 1

8Enyi mataifa, msifuni Mungu wetu, 2 sauti ya sifa yake isikike, 1

9ameyahifadhi maisha yetu 2 na kuizuia miguu yetu kuteleza. 1

10Ee Mungu, wewe ulitujaribu, 2 ukatusafisha kama fedha. 1

11Umetuingiza kwenye nyavu 2 na umetubebesha mizigo mizito 2 migongoni mwetu. 1

12Uliwaruhusu watu watukalie vichwani, 2 tulipita kwenye moto na kwenye maji, 1 lakini ulituleta kwenye nchi 2 iliyojaa utajiri tele. 1

13Nitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwa 2 na kukutimizia nadhiri zangu: 1

14nadhiri ambazo midomo yangu iliahidi 2 na nilizotamka kwa kinywa changu 2 nilipokuwa katika shida. 1

15Nitakutolea dhabihu za wanyama wanono 2 na sadaka za kondoo dume, 2 nitakutolea mafahali na mbuzi. 1

16Njooni msikilize ninyi nyote mnaomcha Mungu, 2 nami niwaambie aliyonitendea. 1

17Nilimlilia kwa kinywa changu, 2 sifa zake zilikuwa katika ulimi wangu. 1

18Kama ningekuwa nimeyaficha maovu moyoni mwangu, 2 Bwana asingekuwa amenisikiliza; 1

19lakini hakika Mungu amenisikiliza 2 na amesikia sauti yangu katika maombi. 1

20Sifa apewe Mungu, 2 ambaye hakulikataa ombi langu 2 wala kunizuilia upendo wake!

← Psalms 65Read In The App, Free →Psalms 67 →

Study Psalms 66

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150