Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 118

1Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; 2 upendo wake wadumu milele. 1

2Israeli na aseme sasa: 2 “Upendo wake wadumu milele.” 1

3Nyumba ya Aroni na iseme sasa: 2 “Upendo wake wadumu milele.” 1

4Wote wamchao Bwana na waseme sasa: 2 “Upendo wake wadumu milele.” 1

5Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana, 2 naye akanijibu kwa kuniweka huru. 1

6Bwana yuko pamoja nami, sitaogopa. 2 Mwanadamu anaweza kunitenda nini? 1

7Bwana yuko pamoja nami, 2 yeye ni msaidizi wangu. 1 Nitawatazama adui zangu 2 wakiwa wameshindwa. 1

8Ni bora kumkimbilia Bwana 2 kuliko kumtumainia mwanadamu. 1

9Ni bora kumkimbilia Bwana 2 kuliko kuwatumainia wakuu. 1

10Mataifa yote yalinizunguka, 2 lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali. 1

11Walinizunguka pande zote, 2 lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali. 1

12Walinizunguka kama kundi la nyuki, 2 lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo; 2 kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali. 1

13Nilisukumwa nyuma karibu kuanguka, 2 lakini Bwana alinisaidia. 1

14Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu, 2 yeye amefanyika wokovu wangu. 1

15Sauti za shangwe na ushindi 2 zinavuma hemani mwa wenye haki: 1 “Mkono wa kuume wa Bwana 2 umetenda mambo makuu! 1

16Mkono wa kuume wa Bwana 2 umeinuliwa juu, 1 mkono wa kuume wa Bwana 2 umetenda mambo makuu!” 1

17Sitakufa, bali nitaishi, 2 nami nitatangaza yale Bwana aliyoyatenda. 1

18Bwana ameniadhibu vikali, 2 lakini hakuniacha nife. 1

19Nifungulie malango ya haki, 2 nami nitaingia na kumshukuru Bwana. 1

20Hili ni lango la Bwana 2 ambalo wenye haki wanaweza kuliingia. 1

21Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, 2 umekuwa wokovu wangu. 1

22Jiwe walilolikataa waashi, 2 limekuwa jiwe kuu la pembeni. 1

23Bwana ametenda hili, 2 nalo ni la kushangaza machoni petu. 1

24Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya, 2 tushangilie na kufurahi ndani yake. 1

25Ee Bwana, tuokoe, 2 Ee Bwana, utujalie mafanikio. 1

26Heri yule ajaye kwa jina la Bwana. 2 Kutoka nyumba ya Bwana tunakubariki. 1

27Bwana ndiye Mungu, 2 naye ametuangazia nuru yake. 1 Mkiwa na matawi mkononi, 2 unganeni kwenye maandamano ya sikukuu 2 hadi kwenye pembe za madhabahu. 1

28Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru, 2 wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza. 1

29Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; 2 upendo wake wadumu milele.

← Psalms 117Read In The App, Free →Psalms 119 →

Study Psalms 118

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150