Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 22

1Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? 2 Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa? 2 Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu? 1

2Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu, 2 hata usiku, sinyamazi. 1

3Hata hivyo umesimikwa katika kiti cha enzi kama Uliye Mtakatifu; 2 wewe ni sifa ya Israeli. + 22:3 Tafsiri zingine zinasema: uketiye juu ya sifa za Israeli. 1

4Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao, 2 walikutumaini nawe ukawaokoa. 1

5Walikulilia wewe na ukawaokoa, 2 walikutegemea wewe nao hawakuaibika. 1

6Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu, 2 wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau. 1

7Wote wanionao hunidhihaki, 2 hunivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao: 1

8Husema, “Anamtegemea Bwana, 2 basi Bwana na amwokoe. 1 Amkomboe basi, kwa maana 2 anapendezwa naye.” 1

9Hata hivyo ulinitoa tumboni, 2 ukanifanya nikutegemee, 1 hata nilipokuwa ninanyonya 2 matiti ya mama yangu. 1

10Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa, 2 toka tumboni mwa mama yangu 2 umekuwa Mungu wangu. 1

11Usiwe mbali nami, 2 kwa maana shida iko karibu 2 na hakuna wa kunisaidia. 1

12Mafahali wengi wamenizunguka, 2 mafahali wa Bashani wenye nguvu 2 wamenizingira. 1

13Simba wangurumao wanaorarua mawindo 2 yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu. 1

14Nimemiminwa kama maji, 2 mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake. 1 Moyo wangu umegeuka kuwa nta, 2 umeyeyuka ndani yangu. 1

15Nguvu zangu zimekauka kama kigae, 2 ulimi wangu umegandamana 2 na kaakaa la kinywa changu, 1 kwa sababu umenilaza 2 katika mavumbi ya kifo. 1

16Mbwa wamenizunguka, 2 kundi la watu waovu limenizingira, 2 wametoboa mikono yangu na miguu yangu. 1

17Naweza kuhesabu mifupa yangu yote, 2 watu wananikodolea macho na kunisimanga. 1

18Wanagawana nguo zangu wao kwa wao, 2 na vazi langu wanalipigia kura. 1

19Lakini wewe, Ee Bwana, 2 usiwe mbali. 1 Ee Nguvu yangu, 2 uje haraka unisaidie. 1

20Okoa maisha yangu na upanga, 2 uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa. 1

21Niokoe kutoka kinywani mwa simba, 2 niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu. 1

22Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, 2 katika kusanyiko nitakusifu wewe. 1

23Ninyi ambao mnamcha Bwana, msifuni! 2 Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye! 2 Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli! 1

24Kwa maana hakupuuza wala kudharau 2 mateso ya aliyeonewa; 1 hakumficha uso wake 2 bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie. 1

25Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa, 2 nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe. 1

26Maskini watakula na kushiba, 2 wale wamtafutao Bwana watamsifu: 2 mioyo yenu na iishi milele! 1

27Miisho yote ya dunia itakumbuka 2 na kumgeukia Bwana, 1 nazo jamaa zote za mataifa 2 watasujudu mbele zake, 1

28kwa maana ufalme ni wa Bwana 2 naye hutawala juu ya mataifa. 1

29Matajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu. 2 Wote waendao mavumbini 2 watapiga magoti mbele yake, 1 wote ambao hawawezi 2 kudumisha uhai wao. 1

30Wazao wa baadaye watamtumikia yeye; 2 vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana. 1

31Watatangaza haki yake kwa watu 2 ambao hawajazaliwa bado, 2 kwa maana yeye ametenda hili.

← Psalms 21Read In The App, Free →Psalms 23 →

Study Psalms 22

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150