Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 51

1Ee Mungu, unihurumie, 2 kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, 1 kwa kadiri ya huruma yako kuu, 2 uyafute makosa yangu. 1

2Unioshe na uovu wangu wote 2 na unitakase dhambi yangu. 1

3Kwa maana ninajua makosa yangu, 2 na dhambi yangu iko mbele yangu daima. 1

4Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi 2 na kufanya yaliyo mabaya machoni pako, 1 ili uthibitike kuwa wa kweli unenapo, 2 na kuwa na haki utoapo hukumu. 1

5Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, 2 mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu. 1

6Hakika wewe wapendezwa na kweli itokayo moyoni, 2 ndani sana ya moyo wangu wanifundisha hekima. 1

7Nioshe kwa hisopo, nami nitakuwa safi, 2 unisafishe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. 1

8Unipe kusikia furaha na shangwe, 2 mifupa uliyoiponda na ifurahi. 1

9Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu, 2 na uufute uovu wangu wote. 1

10Ee Mungu, uniumbie moyo safi, 2 uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu. 1

11Usinitupe kutoka mbele zako 2 wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu. 1

12Unirudishie tena furaha ya wokovu wako, 2 unipe roho ya utii, ili initegemeze. 1

13Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako, 2 na wenye dhambi watakugeukia wewe. 1

14Ee Mungu, Mungu uniokoaye, 2 niokoe na hatia ya kumwaga damu, 2 nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako. 1

15Ee Bwana, fungua midomo yangu, 2 na kinywa changu kitatangaza sifa zako. 1

16Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta, 2 hufurahii sadaka za kuteketezwa. 1

17Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, 2 moyo uliovunjika wenye toba, 2 Ee Mungu, hutaudharau. 1

18Kwa wema wa radhi yako uifanye Sayuni istawi, 2 ukazijenge upya kuta za Yerusalemu. 1

19Hapo ndipo kutakapokuwa na dhabihu za haki, 2 sadaka nzima za kuteketezwa za kukupendeza sana, 1 pia mafahali watatolewa 2 madhabahuni mwako.

← Psalms 50Read In The App, Free →Psalms 52 →

Study Psalms 51

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150