Psalms 71
1Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, 2 usiache nikaaibika kamwe. 1
2Kwa haki yako uniponye na kuniokoa, 2 unitegee sikio lako uniokoe. 1
3Uwe kwangu mwamba wa kimbilio, 2 mahali nitakapokimbilia kila wakati; 1 toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe 2 ni mwamba wangu na ngome yangu. 1
4Ee Mungu wangu uniokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu, 2 kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili. 1
5Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi, 2 tegemeo langu tangu ujana wangu. 1
6Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe, 2 ulinitoa tumboni mwa mama yangu. 2 Nitakusifu wewe daima. 1
7Nimekuwa kama kioja kwa wengi, 2 lakini wewe ni kimbilio langu imara. 1
8Kinywa changu kimejazwa sifa zako, 2 nikitangaza utukufu wako mchana kutwa. 1
9Usinitupe wakati wa uzee, 2 wala usiniache nguvu zangu zinapopungua. 1
10Kwa maana adui zangu wananisengenya, 2 wale wanaonivizia kuniua wafanya hila. 1
11Wanasema, “Mungu amemwacha, 2 mkimbilieni mkamkamate, 2 kwani hakuna wa kumwokoa.” 1
12Ee Mungu, usiwe mbali nami, 2 njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu. 1
13Washtaki wangu na waangamie kwa aibu, 2 wale wanaotaka kunidhuru 2 na wafunikwe kwa dharau na fedheha. 1
14Lakini mimi, nitatumaini siku zote, 2 nitakusifu zaidi na zaidi. 1
15Kinywa changu kitasimulia haki yako, 2 wokovu wako mchana kutwa, 2 ingawa sifahamu kipimo chake. 1
16Ee Bwana Mwenyezi, nitakuja 2 na kutangaza matendo yako makuu, 2 nitatangaza haki yako, yako peke yako. 1
17Ee Mungu, umenifundisha tangu ujana wangu, 2 hadi leo ninatangaza matendo yako ya ajabu. 1
18Ee Mungu, usiniache, 2 hata niwapo mzee wa mvi, 1 mpaka nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho, 2 nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye. 1
19Ee Mungu, haki yako imefika juu katika mbingu, 2 wewe ambaye umefanya mambo makuu. 2 Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe? 1
20Ingawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu, 2 utanihuisha tena, 1 kutoka vilindi vya dunia 2 utaniinua tena. 1
21Utaongeza heshima yangu 2 na kunifariji tena. 1
22Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi 2 kwa ajili ya uaminifu wako; 1 Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli, 2 nitakuimbia sifa kwa zeze. 1
23Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha 2 ninapokuimbia sifa, 2 mimi, ambaye umenikomboa. 1
24Ulimi wangu utasimulia matendo yako ya haki 2 mchana kutwa, 1 kwa maana wale waliotaka kunidhuru, 2 wameaibishwa na kufadhaishwa.