Psalms 78
1Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu, 2 sikilizeni maneno ya kinywa changu. 1
2Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo, 2 nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale: 1
3yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, 2 yale ambayo baba zetu walituambia. 1
4Hatutayaficha kwa watoto wao; 2 tutakiambia kizazi kijacho 1 matendo yastahiliyo sifa ya Bwana, 2 uweza wake, na maajabu aliyoyafanya. 1
5Aliagiza amri kwa Yakobo 2 na akaweka sheria katika Israeli, 1 ambazo aliwaamuru baba zetu 2 wawafundishe watoto wao, 1
6ili kizazi kijacho kizijue, 2 pamoja na watoto ambao watazaliwa, 2 nao pia wapate kuwaeleza watoto wao. 1
7Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu, 2 nao wasingesahau matendo yake, 2 bali wangalizishika amri zake. 1
8Ili wasifanane na baba zao, 2 waliokuwa kizazi cha ukaidi na uasi, 1 ambao roho zao hazikuwa na uaminifu kwake, 2 ambao roho zao hazikumwamini. 1
9Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde, 2 walikimbia siku ya vita. 1
10Hawakulishika agano la Mungu 2 na walikataa kuishi kwa sheria yake. 1
11Walisahau aliyokuwa ameyatenda, 2 maajabu aliyokuwa amewaonyesha. 1
12Alitenda miujiza machoni mwa baba zao, 2 huko Soani, katika nchi ya Misri. 1
13Aliigawanya bahari akawapitisha, 2 alifanya maji yasimame imara kama ukuta. 1
14Aliwaongoza kwa wingu mchana 2 na kwa nuru kutoka kwenye moto usiku kucha. 1
15Alipasua miamba jangwani 2 na akawapa maji tele kama bahari, 1
16alitoa vijito kutoka kwenye jabali lililochongoka, 2 akayafanya maji yatiririke kama mito. 1
17Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake, 2 wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana. 1
18Kwa makusudi walimjaribu Mungu, 2 wakidai vyakula walivyovitamani. 1
19Walinena dhidi ya Mungu, wakisema, 2 “Je, Mungu aweza kuandaa meza jangwani? 1
20Alipopiga mwamba, maji yalitoka kwa nguvu, 2 vijito vikatiririka maji mengi. 1 Lakini je, aweza kutupa chakula pia? 2 Je, anaweza kuwapa watu wake nyama?” 1
21Bwana alipowasikia, alikasirika sana, 2 moto wake ukawa dhidi ya Yakobo, 2 na ghadhabu yake ikawaka dhidi ya Israeli, 1
22kwa kuwa hawakumwamini Mungu, 2 wala kuutumainia ukombozi wake. 1
23Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu 2 na kufungua milango ya mbingu, 1
24akawanyeshea mana ili watu wale; 2 aliwapa nafaka ya mbinguni. 1
25Watu walikula mkate wa malaika, 2 akawatumia chakula chote ambacho wangeliweza kula. 1
26Aliachia upepo wa mashariki kutoka kwenye mbingu 2 na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake. 1
27Aliwanyeshea nyama kama mavumbi, 2 ndege warukao kama mchanga wa pwani. 1
28Aliwafanya washuke ndani ya kambi yao, 2 kuzunguka mahema yao yote. 1
29Walikula na kusaza, 2 kwa maana alikuwa amewapa kile walichotamani. 1
30Kabla hawajamaliza kula walichokitamani, 2 hata kilipokuwa kingali bado vinywani mwao, 1
31hasira ya Mungu ikawaka juu yao, 2 akawaua wale waliokuwa na nguvu zaidi miongoni mwao, 2 akiwaangusha vijana wa Israeli. 1
32Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi, 2 licha ya maajabu yake, hawakuamini. 1
33Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili 2 na miaka yao katika vitisho. 1
34Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, 2 waliosalia walimtafuta, 2 walimgeukia tena kwa shauku. 1
35Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao, 2 kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao. 1
36Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, 2 wakisema uongo kwa ndimi zao, 1
37mioyo yao haikuwa thabiti kwake, 2 wala hawakuwa waaminifu katika agano lake. 1
38Hata hivyo alikuwa na huruma, 2 alisamehe maovu yao 2 na hakuwaangamiza. 1 Mara kwa mara alizuia hasira yake, 2 wala hakuchochea ghadhabu yake yote. 1
39Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, 2 upepo upitao ambao haurudi. 1
40Mara ngapi walimwasi jangwani 2 na kumhuzunisha nyikani! 1
41Walimjaribu Mungu mara kwa mara, 2 wakamkasirisha yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1
42Hawakukumbuka uwezo wake, 2 siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi, 1
43siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri, 2 maajabu yake huko Soani. 1
44Aligeuza mito yao kuwa damu, 2 hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao. 1
45Aliwapelekea makundi ya mainzi yakawala, 2 na vyura wakawaharibu. 1
46Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao, 2 mazao yao kwa nzige. 1
47Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe 2 na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji. 1
48Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe, 2 akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi. 1
49Aliwafungulia hasira yake kali, 2 ghadhabu yake, hasira na uadui, 2 na kundi la malaika wa kuharibu. 1
50Aliitengenezea njia hasira yake, 2 hakuwaepusha na kifo, 2 bali aliwaachia tauni. 1
51Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri, 2 matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu. 1
52Lakini aliwatoa watu wake kama kundi, 2 akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani. 1
53Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa, 2 bali bahari iliwameza adui zao. 1
54Hivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu, 2 hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa. 1
55Aliyafukuza mataifa mbele yao, 2 na kuwagawia nchi zao kama urithi, 2 aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao. 1
56Lakini wao walimjaribu Mungu, 2 na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana, 2 wala hawakuzishika sheria zake. 1
57Kama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu, 2 wakawa wasioweza kutegemewa 2 kama upinde wenye kasoro. 1
58Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu, 2 wakachochea wivu wake kwa sanamu zao. 1
59Wakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana, 2 akamkataa Israeli kabisa. 1
60Akaiacha hema ya Shilo, 2 hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu. 1
61Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani, 2 utukufu wake mikononi mwa adui. 1
62Aliachia watu wake wauawe kwa upanga, 2 akaukasirikia sana urithi wake. 1
63Moto uliwaangamiza vijana wao, 2 na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi, 1
64makuhani wao waliuawa kwa upanga, 2 wala wajane wao hawakuweza kulia. 1
65Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini, 2 kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo. 1
66Aliwapiga na kuwashinda adui zake, 2 akawatia katika aibu ya milele. 1
67Ndipo alipozikataa hema za Yosefu, 2 hakulichagua kabila la Efraimu, 1
68lakini alilichagua kabila la Yuda, 2 Mlima Sayuni, ambao aliupenda. 1
69Alijenga patakatifu pake kama vilele, 2 kama dunia ambayo aliimarisha milele. 1
70Akamchagua Daudi mtumishi wake 2 na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo. 1
71Kutoka kuchunga kondoo alimleta 2 kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo, 2 wa Israeli urithi wake. 1
72Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo, 2 kwa mikono ya ustadi aliwaongoza.