Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 132

1Ee Bwana, mkumbuke Daudi 2 na taabu zote alizozistahimili. 1

2Aliapa kiapo kwa Bwana 2 na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo: 1

3“Sitaingia nyumbani mwangu 2 au kwenda kitandani mwangu: 1

4sitaruhusu usingizi katika macho yangu, 2 wala kope zangu kusinzia, 1

5mpaka nitakapompatia Bwana mahali, 2 makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.” 1

6Tulisikia habari hii huko Efrathi, 2 tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara: + 132:6 Yaani Kiriath-Yearimu. 1

7“Twendeni kwenye makao yake, 2 na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake; 1

8inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia, 2 wewe na Sanduku la nguvu zako. 1

9Makuhani wako na wavikwe haki, 2 watakatifu wako na waimbe kwa furaha.” 1

10Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako, 2 usimkatae mpakwa mafuta wako. 1

11Bwana alimwapia Daudi kiapo, 2 kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua: 1 “Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe 2 katika kiti chako cha enzi, 1

12kama wanao watashika Agano langu 2 na sheria ninazowafundisha, 1 ndipo wana wao watarithi 2 kiti chako cha enzi milele na milele.” 1

13Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni, 2 amepaonea shauku pawe maskani yake: 1

14“Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele; 2 hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, kwa sababu nimepaonea shauku: 1

15Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele: 2 nitashibisha maskini wake kwa chakula. 1

16Nitawavika makuhani wake wokovu, 2 nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha. 1

17“Hapa nitamchipushia Daudi pembe, + 132:17 Pembe inawakilisha nguvu. 2 na kuweka taa kwa ajili ya masiya + 132:17 Masiya yaani mpakwa mafuta. wangu. 1

18Adui zake nitawavika aibu, 2 bali taji kichwani pake itangʼaa sana.”

← Psalms 131Read In The App, Free →Psalms 133 →

Study Psalms 132

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150