Psalms 52
1Ewe jitu, mbona unajivunia ubaya? 2 Kwa nini unajivuna mchana kutwa, 2 wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu? 1
2Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi. 2 Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila. 1
3Unapenda mabaya kuliko mema, 2 uongo kuliko kusema kweli. 1
4Unapenda kila neno lenye kudhuru, 2 ewe ulimi wenye hila! 1
5Hakika Mungu atakushusha chini 2 kwa maangamizi ya milele: 1 atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu 2 kutoka hema yako, 2 atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai. 1
6Wenye haki wataona na kuogopa, 2 watamcheka, wakisema, 1
7“Huyu ni yule mtu ambaye 2 hakumfanya Mungu kuwa ngome yake, 1 bali alitumainia wingi wa utajiri wake, 2 na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!” 1 Neema Ya Mungu 1
8Lakini mimi ni kama mti wa mzeituni 2 unaostawi katika nyumba ya Mungu, 1 nautegemea upendo wa Mungu usiokoma 2 milele na milele. 1
9Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda, 2 nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema. 2 Nitakusifu mbele ya watakatifu wako.