Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 38

1Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, 2 wala kuniadhibu katika ghadhabu yako. 1

2Kwa kuwa mishale yako imenichoma, 2 na mkono wako umenishukia. 1

3Hakuna afya mwilini mwangu 2 kwa sababu ya ghadhabu yako, 1 mifupa yangu haina uzima 2 kwa sababu ya dhambi zangu. 1

4Maovu yangu yamenifunika 2 kama mzigo usiochukulika. 1

5Majeraha yangu yameoza na yananuka, 2 kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu. 1

6Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, 2 mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. 1

7Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, 2 hakuna afya mwilini mwangu. 1

8Nimedhoofika na kupondwa kabisa, 2 nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni. 1

9Ee Bwana, yote ninayoyaonea shauku 2 yako wazi mbele zako, 1 kutamani kwangu sana 2 hakufichiki mbele zako. 1

10Moyo wangu unapigapiga, 2 nguvu zangu zimeniishia; 2 hata macho yangu yametiwa giza. 1

11Rafiki na wenzangu wananikwepa 2 kwa sababu ya majeraha yangu; 2 majirani zangu wanakaa mbali nami. 1

12Wale wanaotafuta uhai wangu 2 wanatega mitego yao, 1 wale ambao wangetaka kunidhuru 2 huongea juu ya maangamizi yangu; 2 hufanya shauri la hila mchana kutwa. 1

13Mimi ni kama mtu kiziwi, asiyeweza kusikia, 2 ni kama bubu, asiyeweza kufungua kinywa chake, 1

14nimekuwa kama mtu asiyesikia, 2 ambaye kinywa chake hakiwezi kutoa jibu. 1

15Ee Bwana, ninakungojea wewe, 2 Ee Bwana Mungu wangu, utajibu. 1

16Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, 2 wala wasijitukuze juu yangu 2 mguu wangu unapoteleza.” 1

17Kwa maana ninakaribia kuanguka, 2 na maumivu yangu yananiandama siku zote. 1

18Naungama uovu wangu, 2 ninataabishwa na dhambi yangu. 1

19Wengi ni wale ambao ni adui zangu hodari, 2 wale wanaonichukia bila sababu ni wengi. 1

20Wanaolipa maovu kwa wema wangu 2 hunisingizia ninapofuata lililo jema. 1

21Ee Bwana, usiniache, 2 usiwe mbali nami, Ee Mungu wangu. 1

22Ee Bwana Mwokozi wangu, 2 uje upesi kunisaidia.

← Psalms 37Read In The App, Free →Psalms 39 →

Study Psalms 38

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150