Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 79

1Ee Mungu, mataifa yameuvamia urithi wako, 2 wamelinajisi Hekalu lako takatifu, 2 wameifanya Yerusalemu kuwa magofu. 1

2Wametoa maiti za watumishi 2 kuwa chakula cha ndege wa angani 1 na nyama ya watakatifu wako 2 kwa wanyama wa nchi. 1

3Wamemwaga damu kama maji 2 kuzunguka Yerusalemu yote, 2 wala hakuna yeyote wa kuwazika. 1

4Tumekuwa kitu cha aibu kwa jirani zetu, 2 cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka. 1

5Hata lini, Ee Bwana? Je, wewe utakasirika milele? 2 Wivu wako utawaka kama moto hadi lini? 1

6Mwaga ghadhabu yako kwa mataifa yasiyokukubali, 2 juu ya falme za hao wasioliitia jina lako, 1

7kwa maana wamemrarua Yakobo 2 na kuharibu nchi ya makao yake. 1

8Usituhesabie dhambi za baba zetu, 2 huruma yako na itujie hima, 2 kwa maana tu wahitaji mno. 1

9Ee Mungu Mwokozi wetu, utusaidie, 2 kwa ajili ya utukufu wa jina lako; 1 tuokoe na kutusamehe dhambi zetu 2 kwa ajili ya jina lako. 1

10Kwa nini mataifa waseme, 2 “Yuko wapi Mungu wenu?” 1 Mbele ya macho yetu, 2 dhihirisha kati ya mataifa 1 kwamba unalipiza kisasi damu iliyomwagwa 2 ya watumishi wako. 1

11Kilio cha huzuni cha wafungwa kifike mbele zako; 2 kwa nguvu za mkono wako 2 hifadhi wale waliohukumiwa kufa. 1

12Walipize jirani zetu mara saba vifuani mwao 2 aibu walizovurumisha juu yako, Ee Bwana. 1

13Ndipo sisi watu wako, kondoo wa malisho yako, 2 tutakusifu milele; 1 toka kizazi hadi kizazi 2 tutasimulia sifa zako.

← Psalms 78Read In The App, Free →Psalms 80 →

Study Psalms 79

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150