Psalms 44
1Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, 2 baba zetu wametueleza 1 yale uliyotenda katika siku zao, 2 siku za kale. 1
2Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa 2 na ukawapanda baba zetu, 1 uliangamiza mataifa 2 na kuwastawisha baba zetu. 1
3Sio kwa upanga wao waliipata nchi, 2 wala si mkono wao uliwapatia ushindi; 1 ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, 2 na nuru ya uso wako, 2 kwa kuwa uliwapenda. 1
4Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu, 2 unayeamuru ushindi kwa Yakobo. 1
5Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu; 2 kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu. 1
6Siutumaini upinde wangu, 2 upanga wangu hauniletei ushindi; 1
7bali wewe unatupa ushindi juu ya adui zetu, 2 unawaaibisha watesi wetu. 1
8Katika Mungu wetu tunajivuna mchana kutwa, 2 nasi tutalisifu jina lako milele. 1
9Lakini sasa umetukataa na kutudhili, 2 wala huendi tena na jeshi letu. 1
10Umetufanya turudi nyuma mbele ya adui, 2 nao watesi wetu wametuteka nyara. 1
11Umetuacha tutafunwe kama kondoo 2 na umetutawanya katika mataifa. 1
12Umewauza watu wako kwa fedha kidogo, 2 wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao. 1
13Umetufanya lawama kwa jirani zetu, 2 dharau na dhihaka kwa wale wanaotuzunguka. 1
14Umetufanya kuwa mithali miongoni mwa mataifa, 2 mataifa hutikisa vichwa vyao. 1
15Fedheha yangu iko mbele yangu mchana kutwa, 2 na uso wangu umejaa aibu tele, 1
16kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana, 2 kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi. 1
17Hayo yote yametutokea, 2 ingawa tulikuwa hatujakusahau 2 wala hatujaenda kinyume na agano lako. 1
18Mioyo yetu ilikuwa haijarudi nyuma; 2 nyayo zetu zilikuwa hazijaiacha njia yako. 1
19Lakini ulituponda na kutufanya makao ya mbweha, 2 na ukatufunika kwa giza nene. 1
20Kama tungalikuwa tumelisahau jina la Mungu wetu 2 au kunyooshea mikono yetu kwa mungu mgeni, 1
21je, Mungu hangaligundua hili, 2 kwa kuwa anazijua siri za moyo? 1
22Hata hivyo kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; 2 tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa. 1
23Amka, Ee Bwana! Kwa nini unalala? 2 Zinduka! Usitukatae milele. 1
24Kwa nini unauficha uso wako 2 na kusahau taabu na mateso yetu? 1
25Tumeshushwa hadi mavumbini, 2 miili yetu imegandamana na ardhi. 1
26Inuka na utusaidie, 2 utukomboe kwa sababu ya upendo wako usio na mwisho.