Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 147

1Msifuni Bwana. 1 Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa, 2 jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye! 1

2Bwana hujenga Yerusalemu, 2 huwakusanya Israeli walio uhamishoni. 1

3Anawaponya waliovunjika mioyo 2 na kuvifunga vidonda vyao. 1

4Huzihesabu nyota 2 na huipa kila moja jina lake. 1

5Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, 2 ufahamu wake hauna kikomo. 1

6Bwana huwahifadhi wanyenyekevu 2 lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini. 1

7Mwimbieni Bwana kwa shukrani, 2 mpigieni Mungu wetu kinubi. 1

8Yeye huzifunika anga kwa mawingu, 2 huinyeshea ardhi mvua, 2 na kuzifanya nyasi kuota juu ya vilima. 1

9Huwapa chakula mifugo 2 na pia makinda ya kunguru yanapolia. 1

10Furaha yake haipo katika nguvu za farasi, 2 wala furaha yake kwenye miguu ya mwanadamu. 1

11Bwana hupendezwa na wale wamchao, 2 wale wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usiokoma. 1

12Mtukuze Bwana, ee Yerusalemu, 2 msifu Mungu wako, ee Sayuni, 1

13kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako 2 na huwabariki watu wako walio ndani yako. 1

14Huwapa amani mipakani mwenu 2 na kukushibisha kwa ngano safi kabisa. 1

15Hutuma amri yake duniani, 2 neno lake hukimbia kasi. 1

16Anatandaza theluji kama sufu 2 na kutawanya umande kama majivu. 1

17Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe. 2 Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake? 1

18Hutuma neno lake na kuviyeyusha, 2 huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka. 1

19Amemfunulia Yakobo neno lake, 2 sheria zake na maagizo yake kwa Israeli. 1

20Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote, 2 hawazijui sheria zake. 1 Msifuni Bwana.

← Psalms 146Read In The App, Free →Psalms 148 →

Study Psalms 147

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150