Psalms 109
1Ee Mungu, ambaye ninakusifu, 2 usiwe kimya, 1
2kwa maana watu waovu na wadanganyifu 2 wamefungua vinywa vyao dhidi yangu; 1 wasema dhidi yangu 2 kwa ndimi za udanganyifu. 1
3Wamenizunguka kwa maneno ya chuki, 2 wananishambulia bila sababu. 1
4Wanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki, 2 lakini mimi ninawaombea. 1
5Wananilipiza mabaya kwa mema, 2 chuki badala ya urafiki wangu. 1
6Agiza mtu mwovu ampinge, 2 mshtaki + 109:6 Mshtaki hapa maana yake ni Shetani. asimame mkono wake wa kuume. 1
7Anapohukumiwa, apatikane na hatia, 2 nayo maombi yake yamhukumu. 1
8Siku zake za kuishi na ziwe chache, 2 nafasi yake ya uongozi ichukuliwe na mtu mwingine. 1
9Watoto wake na waachwe yatima, 2 mke wake na awe mjane. 1
10Watoto wake na watangetange wakiomba, 2 na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao. 1
11Mtu anayemdai na ateke vyote alivyo navyo, 2 matunda ya kazi yake yatekwe nyara na wageni. 1
12Asiwepo mtu yeyote wa kumtendea mema 2 wala wa kuwahurumia yatima wake. 1
13Uzao wake na ukatiliwe mbali, 2 majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho. 1
14Maovu ya baba zake na yakumbukwe 2 mbele za Bwana, 1 dhambi ya mama yake 2 isifutwe kamwe. 1
15Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana, 2 ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani. 1
16Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema, 2 bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, 2 aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo. 1
17Alipenda kulaani, 2 nayo laana ikampata; 1 hakupenda kubariki, 2 kwa hiyo baraka na ikae mbali naye. 1
18Alivaa kulaani kama vazi lake, 2 nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji, 2 kwenye mifupa yake kama mafuta. 1
19Na iwe kama joho alilozungushiwa, 2 kama mshipi aliofungiwa daima. 1
20Haya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu, 2 kwa wale wanaoninenea mabaya. 1
21Lakini wewe, Ee Bwana Mwenyezi, 2 unitendee wema kwa ajili ya jina lako, 2 uniokoe kwa wema wa pendo lako. 1
22Maana mimi ni maskini na mhitaji, 2 moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu. 1
23Ninafifia kama kivuli cha jioni, 2 nimerushwa-rushwa kama nzige. 1
24Magoti yangu yamelegea kwa kufunga, 2 mwili wangu umedhoofika na kukonda. 1
25Nimekuwa kitu cha kudharauliwa kwa washtaki wangu, 2 wanionapo, hutikisa vichwa vyao. 1
26Ee Bwana, Mungu wangu nisaidie, 2 niokoe sawasawa na upendo wako. 1
27Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako, 2 kwamba wewe, Ee Bwana, umetenda hili. 1
28Wanaweza kulaani, lakini wewe utabariki, 2 watakaposhambulia wataaibishwa, 2 lakini mtumishi wako atashangilia. 1
29Washtaki wangu watavikwa fedheha, 2 na kufunikwa na aibu kama joho. 1
30Kwa kinywa changu nitamtukuza sana Bwana, 2 katika umati mkubwa nitamsifu. 1
31Kwa maana husimama mkono wa kuume wa mhitaji, 2 kuokoa maisha yake kutoka kwa wale wanaomhukumu.