Psalms 107
1Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema, 2 upendo wake wadumu milele. 1
2Waliokombolewa wa Bwana na waseme hivi, 2 wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui, 1
3wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali, 2 kutoka mashariki na magharibi, 2 kutoka kaskazini na kusini. 1
4Baadhi yao walitangatanga jangwani, 2 hawakuona njia ya kuwafikisha mji ambao wangeweza kuishi. 1
5Walikuwa na njaa na kiu, 2 nafsi zao zikadhoofika. 1
6Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, 2 naye akawaokoa kutoka taabu yao. 1
7Akawaongoza kwa njia iliyo sawa 2 hadi mji ambao wangeweza kuishi. 1
8Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, 2 na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu, 1
9kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu, 2 na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema. 1
10Wengine walikaa gizani na katika huzuni kuu, 2 wafungwa wakiteseka katika minyororo, 1
11kwa sababu walikuwa wameasi 2 dhidi ya maneno ya Mungu 1 na kudharau shauri 2 la Aliye Juu Sana. 1
12Aliwatumikisha kwa kazi ngumu; 2 walijikwaa na hapakuwepo yeyote wa kuwasaidia. 1
13Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, 2 naye akawaokoa kutoka taabu yao. 1
14Akawatoa katika giza na huzuni kuu 2 na akavunja minyororo yao. 1
15Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, 2 na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu, 1
16kwa kuwa yeye huvunja malango ya shaba 2 na kukata mapingo ya chuma. 1
17Wengine wakawa wapumbavu kutokana na uasi wao, 2 wakapata mateso kwa sababu ya uovu wao. 1
18Wakachukia kabisa vyakula vyote, 2 wakakaribia malango ya mauti. 1
19Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, 2 naye akawaokoa kutoka taabu yao. 1
20Akalituma neno lake na kuwaponya, 2 akawaokoa kutoka maangamizo yao. 1
21Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, 2 na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. 1
22Na watoe dhabihu za kushukuru, 2 na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha. 1
23Wengine walisafiri baharini kwa meli, 2 walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu. 1
24Waliziona kazi za Bwana, 2 matendo yake ya ajabu kilindini. 1
25Kwa maana alisema na kuamsha tufani 2 iliyoinua mawimbi juu. 1
26Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini, 2 katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka. 1
27Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi, 2 ujanja wao ukafikia ukomo. 1
28Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao, 2 naye akawatoa kwenye taabu yao. 1
29Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono, 2 mawimbi ya bahari yakatulia. 1
30Walifurahi ilipokuwa shwari, 2 naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani. 1
31Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma, 2 na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. 1
32Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, 2 na wamsifu katika baraza la wazee. 1
33Yeye aligeuza mito kuwa jangwa, 2 chemchemi za maji zitiririkazo kuwa ardhi yenye kiu, 1
34nchi izaayo ikawa ya chumvi isiyofaa, 2 kwa sababu ya uovu wa wale walioishi humo. 1
35Aligeuza jangwa likawa madimbwi ya maji, 2 nayo ardhi kame kuwa chemchemi za maji zitiririkazo; 1
36aliwaleta wenye njaa wakaishi humo, 2 nao wakajenga mji wangeweza kuishi. 1
37Walilima mashamba na kupanda mizabibu, 2 nayo ikazaa matunda mengi, 1
38Mungu aliwabariki, hesabu yao ikaongezeka sana, 2 wala hakuruhusu mifugo yao kupungua. 1
39Kisha hesabu yao ilipungua, na walinyenyekeshwa 2 kwa kuonewa, maafa na huzuni. 1
40Yeye ambaye huwamwagia dharau wakuu, 2 aliwafanya watangetange nyikani isiyo na njia. 1
41Lakini yeye aliwainua wahitaji katika taabu zao, 2 na kuongeza jamaa zao kama makundi ya kondoo. 1
42Wanyofu wataona na kufurahi, 2 lakini waovu wote watafunga vinywa vyao. 1
43Yeyote aliye na hekima, ayasikie mambo haya, 2 na atafakari upendo mkuu wa Bwana.