Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 139

1Ee Bwana, umenichunguza 2 na kunijua. 1

2Unajua ninapoketi na ninapoinuka; 2 unatambua mawazo yangu tokea mbali. 1

3Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; 2 unaelewa njia zangu zote. 1

4Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, 2 wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana. 1

5Umenizunguka nyuma na mbele; 2 umeweka mkono wako juu yangu. 1

6Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu, 2 ni ya juu sana kwangu kuyafikia. 1

7Niende wapi nijiepushe na Roho yako? 2 Niende wapi niukimbie uso wako? 1

8Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; 2 nikifanya vilindi + 139:8 Vilindi ina maana ya Kuzimu, ambayo ni Sheol kwa Kiebrania. kuwa kitanda changu, 2 wewe uko huko. 1

9Kama nikipanda juu ya mbawa za mapambazuko, 2 kama nikikaa pande za mbali za bahari, 1

10hata huko mkono wako utaniongoza, 2 mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti. 1

11Kama nikisema, “Hakika giza litanificha 2 na nuru inayonizunguka iwe usiku,” 1

12hata giza halitakuwa giza kwako, 2 usiku utangʼaa kama mchana, 2 kwa kuwa giza ni kama nuru kwako. 1

13Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani; 2 uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu. 1

14Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa 2 kwa namna ya ajabu na ya kutisha; 1 kazi zako ni za ajabu, 2 ninajua hayo kikamilifu. 1

15Umbile langu halikufichika kwako, 2 nilipoumbwa mahali pa siri. 1 Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi, 2

16macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika. 1 Siku zangu zote ulizonipangia 2 ziliandikwa katika kitabu chako 2 kabla haijakuwepo hata moja. 1

17Tazama jinsi yalivyo ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu! 2 Jinsi jumla yake ilivyo kubwa! 1

18Kama ningezihesabu, 2 zingekuwa nyingi kuliko mchanga. 1 Niamkapo, 2 bado niko pamoja nawe. 1

19Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu! 2 Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu! 1

20Wanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya, 2 adui zako wanatumia vibaya jina lako. 1

21Ee Bwana, je, nisiwachukie wanaokuchukia? 2 Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako? 1

22Sina kitu zaidi ya chuki dhidi yao, 2 ninawahesabu ni adui zangu. 1

23Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, 2 nijaribu na ujue mawazo yangu. 1

24Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, 2 uniongoze katika njia ya milele.

← Psalms 138Read In The App, Free →Psalms 140 →

Study Psalms 139

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150