Psalms 17
1Sikia, Ee Bwana, kusihi kwangu kwa haki, 2 sikiliza kilio changu. 1 Tega sikio kwa ombi langu, 2 halitoki kwenye midomo ya udanganyifu. 1
2Hukumu yangu na itoke kwako, 2 macho yako na yaone yale yaliyo haki. 1
3Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, 2 ingawa umenijaribu, hutaona chochote. 1 Nimeamua kwamba kinywa changu 2 hakitatenda dhambi. 1
4Kuhusu matendo ya wanadamu: 2 kwa neno la midomo yako, 1 nimejiepusha 2 na njia za wenye jeuri. 1
5Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; 2 nyayo zangu hazikuteleza. 1
6Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, 2 nitegee sikio lako na usikie ombi langu. 1
7Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, 2 wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume 2 wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao. 1
8Nilinde kama mboni ya jicho lako, 2 unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako 1
9kutokana na waovu wanaonishambulia, 2 kutokana na adui wauaji wanaonizunguka. 1
10Huifunga mioyo yao iliyo migumu, 2 vinywa vyao hunena kwa majivuno. 1
11Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira, 2 wakiwa macho, waniangushe chini. 1
12Wamefanana na simba mwenye njaa awindaye, 2 kama simba mkubwa anyemeleaye mafichoni. 1
13Inuka, Ee Bwana, pambana nao, uwaangushe, 2 niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako. 1
14Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, 2 kutokana na watu wa ulimwengu huu 2 ambao fungu lao liko katika maisha haya. 1 Na wapate adhabu ya kuwatosha. 2 Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, 2 hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao. 1
15Na mimi katika haki nitauona uso wako, 2 niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.