Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 108

1Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; 2 nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. 1

2Amka, kinubi na zeze! 2 Nitayaamsha mapambazuko. 1

3Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; 2 nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu. 1

4Kwa maana upendo wako ni mkuu, ni juu kuliko mbingu; 2 uaminifu wako unazifikia anga. 1

5Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, 2 utukufu wako na uenee duniani kote. 1

6Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume, 2 ili wale uwapendao wapate kuokolewa. 1

7Mungu amenena kutoka patakatifu pake: 2 “Nitaigawa Shekemu kwa ushindi 2 na kulipima Bonde la Sukothi. 1

8Gileadi ni yangu, Manase ni yangu, 2 Efraimu ni kofia yangu ya chuma, 2 nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala. 1

9Moabu ni sinia langu la kunawia, 2 juu ya Edomu natupa kiatu changu; 2 nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.” 1

10Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome? 2 Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu? 1

11Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi, 2 na hutoki tena na majeshi yetu? 1

12Tuletee msaada dhidi ya adui, 2 kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu. 1

13Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi, 2 naye atawaponda adui zetu.

← Psalms 107Read In The App, Free →Psalms 109 →

Study Psalms 108

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150