Psalms 42
1Kama vile ayala aoneavyo shauku vijito vya maji, 2 ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu. 1
2Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai. 2 Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu? 1
3Machozi yangu yamekuwa chakula changu 2 usiku na mchana, 1 huku watu wakiniambia mchana kutwa, 2 “Yuko wapi Mungu wako?” 1
4Mambo haya nayakumbuka 2 ninapoimimina nafsi yangu: 1 Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu, 2 nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu, 1 kwa kelele za shangwe na za shukrani 2 katikati ya umati uliosherehekea. 1
5Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? 2 Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? 1 Weka tumaini lako kwa Mungu, 2 kwa sababu bado nitamsifu, 2 Mwokozi wangu na
6Mungu wangu. 1 Nafsi yangu inasononeka ndani yangu; 2 kwa hiyo nitakukumbuka 1 kutoka nchi ya Yordani, 2 katika vilele vya Hermoni, 2 kutoka Mlima Mizari. 1
7Kilindi huita kilindi, 2 katika ngurumo za maporomoko ya maji yako; 1 mawimbi yako yote pamoja na viwimbi 2 vimepita juu yangu. 1
8Mchana Bwana huelekeza upendo wake, 2 usiku wimbo wake uko nami: 2 maombi kwa Mungu wa uzima wangu. 1
9Ninamwambia Mungu Mwamba wangu, 2 “Kwa nini umenisahau? 1 Kwa nini niendelee kuomboleza, 2 nikiwa nimeonewa na adui?” 1
10Mifupa yangu inateseka kwa maumivu makali 2 adui zangu wanaponidhihaki, 1 wakiniambia mchana kutwa, 2 “Yuko wapi Mungu wako?” 1
11Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka? 2 Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu? 1 Weka tumaini lako kwa Mungu, 2 kwa sababu bado nitamsifu, 2 Mwokozi wangu na Mungu wangu.