Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 105

1Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake, 2 wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. 1

2Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa, 2 waambieni matendo yake yote ya ajabu. 1

3Lishangilieni jina lake takatifu, 2 mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi. 1

4Mtafuteni Bwana na nguvu zake, 2 utafuteni uso wake siku zote. 1

5Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, 2 miujiza yake na hukumu alizozitamka, 1

6enyi wazao wa Abrahamu mtumishi wake, 2 enyi wana wa Yakobo, wateule wake. 1

7Yeye ndiye Bwana Mungu wetu, 2 hukumu zake zimo duniani pote. 1

8Hulikumbuka agano lake milele, 2 neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu, 1

9agano alilolifanya na Abrahamu, 2 kiapo alichomwapia Isaki. 1

10Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, 2 kwa Israeli liwe agano la milele: 1

11“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani 2 kuwa sehemu utakayoirithi.” 1

12Walipokuwa wachache kwa idadi, 2 wachache sana na wageni ndani yake, 1

13walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, 2 kutoka ufalme mmoja hadi mwingine. 1

14Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; 2 kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema: 1

15“Msiwaguse niliowatia mafuta; 2 msiwadhuru manabii wangu.” 1

16Akaiita njaa juu ya nchi 2 na kuharibu chakula chao chote, 1

17naye akatuma mtu mbele yao, 2 Yosefu, aliyeuzwa kama mtumwa. 1

18Walichubua miguu yake kwa minyororo, 2 shingo yake ilifungwa kwa chuma, 1

19hadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia, 2 hadi neno la Bwana lilipomthibitisha. 1

20Mfalme alituma watu wakamfungua, 2 mtawala wa watu alimwachia huru. 1

21Alimfanya mkuu wa nyumba yake, 2 mtawala juu ya vyote alivyokuwa navyo, 1

22kuwaelekeza wakuu wa mfalme apendavyo 2 na kuwafundisha wazee wake hekima. 1

23Kisha Israeli akaingia Misri, 2 Yakobo akaishi kama mgeni katika nchi ya Hamu. 1

24Bwana aliwafanya watu wake kuzaana sana, 2 akawafanya kuwa wengi sana kuliko adui zao, 1

25ndiye aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake, 2 wakatenda hila dhidi ya watumishi wake. 1

26Akamtuma Mose mtumishi wake, 2 pamoja na Aroni, aliyemchagua. 1

27Walifanya ishara zake za ajabu miongoni mwao, 2 miujiza yake katika nchi ya Hamu. 1

28Alituma giza na nchi ikajaa giza, 2 kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake? 1

29Aligeuza maji yao kuwa damu, 2 ikasababisha samaki wao kufa. 1

30Nchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia 2 hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao. 1

31Alisema, yakaja makundi ya mainzi, 2 na viroboto katika nchi yao yote. 1

32Alibadilisha mvua yao ikawa mvua ya mawe, 2 yenye umeme wa radi nchini yao yote, 1

33akaharibu mizabibu yao na miti ya tini, 2 na akaangamiza miti ya nchi yao. 1

34Alisema, nzige wakaja, 2 tunutu wasio na idadi, 1

35wakala kila jani katika nchi yao, 2 wakala mazao ya ardhi yao. 1

36Kisha akawaua wazaliwa wote wa kwanza katika nchi yao, 2 matunda ya kwanza ya ujana wao wote. 1

37Akawatoa Israeli katika nchi 2 wakiwa na fedha na dhahabu nyingi, 1 wala hakuna hata mmoja 2 kutoka kabila zao aliyejikwaa. 1

38Misri ilifurahi walipoondoka, 2 kwa sababu hofu ya Israeli ilikuwa imewaangukia. 1

39Alitandaza wingu kama kifuniko, 2 na moto kuwamulikia usiku. 1

40Waliomba, naye akawaletea kware, 2 akawashibisha kwa mkate wa mbinguni. 1

41Alipasua mwamba, maji yakabubujika, 2 yakatiririka jangwani kama mto. 1

42Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu, 2 aliyompa Abrahamu mtumishi wake. 1

43Aliwatoa watu wake kwa furaha, 2 wateule wake kwa kelele za shangwe, 1

44akawapa nchi za mataifa, wakawa warithi 2 wa mali wengine walikuwa wameitaabikia: 1

45alifanya haya ili wayashike mausia yake 2 na kuzitii sheria zake. 1 Msifuni Bwana. + 105:45 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.

← Psalms 104Read In The App, Free →Psalms 106 →

Study Psalms 105

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150