Psalms 106
1Msifuni Bwana. 1 Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema; 2 upendo wake wadumu milele. 1
2Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya Bwana 2 au kutangaza kikamilifu sifa zake? 1
3Heri wale wanaodumisha haki, 2 ambao daima wanafanya yaliyo mema. 1
4Ee Bwana, unikumbuke unapowatendea mema watu wako, 2 uwe msaada wangu unapowaokoa, 1
5ili niweze kufurahia mafanikio ya wateule wako, 2 niweze kushiriki katika furaha ya taifa lako, 2 na kuungana na urithi wako katika kukusifu. 1
6Tumetenda dhambi, kama vile baba zetu walivyotenda, 2 tumekosa na tumetenda uovu. 1
7Wakati baba zetu walipokuwa Misri, 2 hawakuzingatia maajabu yako, 1 wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako, 2 bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu. 1
8Hata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake, 2 ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu. 1
9Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka, 2 akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani. 1
10Aliwaokoa mikononi mwa adui; 2 kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa. 1
11Maji yaliwafunika adui zao, 2 hakunusurika hata mmoja. 1
12Ndipo walipoamini ahadi zake, 2 nao wakaimba sifa zake. 1
13Lakini mara walisahau aliyowatendea, 2 wala hawakungojea shauri lake. 1
14Jangwani walitawaliwa na tamaa zao, 2 walimjaribu Mungu nyikani. 1
15Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba, 2 lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha. 1
16Kambini walimwonea wivu Mose, 2 na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana. 1
17Ardhi ilifunguka ikawameza Dathani, 2 ikawazika Abiramu na kundi lake. 1
18Moto uliwaka katikati ya wafuasi wao, 2 mwali wa moto uliwateketeza waovu. 1
19Huko Horebu walitengeneza ndama, 2 na kuabudu sanamu ya kusubu kwa chuma. 1
20Waliubadilisha Utukufu wao 2 kwa sanamu ya fahali, ambaye hula majani. 1
21Walimsahau Mungu aliyewaokoa, 2 aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri, 1
22miujiza katika nchi ya Hamu 2 na mambo ya kutisha huko Bahari ya Shamu. 1
23Kwa hiyo alisema kwamba angewaangamiza: 2 kama Mose mteule wake, 1 asingesimama kati yao na Mungu 2 kuizuia ghadhabu yake kuwaangamiza. 1
24Kisha waliidharau ile nchi nzuri, 2 hawakuiamini ahadi yake. 1
25Walinungʼunika ndani ya mahema yao, 2 wala hawakumtii Bwana. 1
26Kwa hiyo akaapa kwa mkono ulioinuliwa 2 kwamba atawafanya waanguke jangwani, 1
27kuwatawanya wazao wao waanguke miongoni mwa mataifa, 2 na kuwatawanya katika nchi zote. 1
28Walijifunga nira na Baali wa Peori, 2 wakala dhabihu zilizotolewa kwa miungu isiyo na uhai. 1
29Waliichochea hasira ya Bwana, 2 wakamkasirisha kwa matendo yao maovu, 2 nayo tauni ikazuka katikati yao. 1
30Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati, 2 nayo tauni ikazuiliwa. 1
31Hili likahesabiwa kwake haki, 2 kwa vizazi visivyo na mwisho vijavyo. 1
32Kwenye maji ya Meriba, walimkasirisha Bwana, 2 janga likampata Mose kwa sababu yao; 1
33kwa maana walimwasi Roho wa Mungu, 2 na maneno yasiyofaa yakatoka midomoni kwa Mose. 1
34Hawakuyaangamiza yale mataifa 2 kama Bwana alivyowaagiza, 1
35bali walijichanganya na mataifa 2 na wakazikubali desturi zao. 1
36Waliabudu sanamu zao, 2 zikawa mtego kwao. 1
37Wakawatoa wana wao 2 na binti zao dhabihu kwa mashetani. 1
38Walimwaga damu isiyo na hatia, 2 damu za wana wao na binti zao, 1 ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani, 2 nayo nchi ikanajisika kwa damu zao. 1
39Wakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda; 2 kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba. 1
40Kwa hiyo Bwana akawakasirikia watu wake 2 na akauchukia sana urithi wake. 1
41Akawakabidhi kwa mataifa 2 na adui zao wakawatawala. 1
42Adui zao wakawaonea 2 na kuwatia chini ya mamlaka yao. 1
43Mara nyingi aliwaokoa 2 lakini walikuwa wamezama kwenye uasi, 2 nao wakajiharibu katika dhambi zao. 1
44Lakini akaangalia mateso yao 2 wakati aliposikia kilio chao; 1
45kwa ajili yao akakumbuka agano lake, 2 na kutokana na upendo wake mkuu akapooza hasira yake. 1
46Akawafanya wahurumiwe 2 na wote waliowashikilia mateka. 1
47Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe. 2 Tukusanye tena kutoka kwa mataifa, 1 ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, 2 na kushangilia katika sifa zako. 1
48Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, 2 tangu milele na hata milele. 1 Watu wote na waseme, “Amen!” 1 Msifuni Bwana.