Psalms 37
1Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu, 2 wala usiwaonee wivu watendao mabaya, 1
2kwa maana kama majani watanyauka mara, 2 kama mimea ya kijani watakufa mara. 1
3Mtumaini Bwana na utende yaliyo mema; 2 Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama. 1
4Jifurahishe katika Bwana 2 naye atakupa haja za moyo wako. 1
5Mkabidhi Bwana njia yako, 2 mtumaini yeye, naye atatenda hili: 1
6Yeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko, 2 na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri. 1
7Tulia mbele za Bwana 2 na umngojee kwa uvumilivu; 1 usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao, 2 wanapotekeleza mipango yao miovu. 1
8Epuka hasira na uache ghadhabu, 2 usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu. 1
9Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, 2 bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi. 1
10Bado kitambo kidogo, nao waovu hawataonekana, 2 ingawa utawatafuta, hawataonekana. 1
11Bali wanyenyekevu watairithi nchi 2 na wafurahie amani tele. 1
12Waovu hula njama dhidi ya wenye haki 2 na kuwasagia meno, 1
13bali Bwana huwacheka waovu, 2 kwa sababu anajua siku yao inakuja. 1
14Waovu huchomoa upanga 2 na kupinda upinde, 1 ili wawaangushe maskini na wahitaji, 2 kuwachinja wale ambao njia zao ni nyofu. 1
15Lakini panga zao zitachoma mioyo yao wenyewe, 2 na pinde zao zitavunjwa. 1
16Bora kidogo walicho nacho wenye haki 2 kuliko wingi wa mali wa waovu wengi; 1
17kwa maana nguvu za waovu zitavunjwa, 2 lakini Bwana humtegemeza mwenye haki. 1
18Bwana anazifahamu siku za wanyofu, 2 na urithi wao utadumu milele. 1
19Siku za maafa hawatanyauka, 2 siku za njaa watafurahia wingi wa vitu. 1
20Lakini waovu wataangamia: 2 Adui za Bwana watakuwa 2 kama uzuri wa mashamba, 1 watatoweka, 2 watatoweka kama moshi. 1
21Waovu hukopa na hawalipi, 2 bali wenye haki hutoa kwa ukarimu. 1
22Wale wanaobarikiwa na Bwana watairithi nchi, 2 bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali. 1
23Kama Bwana akipendezwa na njia ya mtu, 2 yeye huimarisha hatua zake, 1
24ajapojikwaa, hataanguka, 2 kwa maana Bwana 2 humtegemeza kwa mkono wake. 1
25Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, 2 lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa 2 au watoto wao wakiombaomba chakula. 1
26Wakati wote ni wakarimu na hukopesha bila masharti. 2 Watoto wao watabarikiwa. 1
27Acha ubaya na utende wema, 2 nawe utaishi katika nchi milele. 1
28Kwa kuwa Bwana huwapenda wenye haki 2 naye hatawaacha waaminifu wake. 1 Watalindwa milele, 2 lakini uzao wa waovu utakatiliwa mbali. 1
29Wenye haki watairithi nchi, 2 na kuishi humo milele. 1
30Kinywa cha mwenye haki hutamka hekima, 2 nao ulimi wake huzungumza lililo haki. 1
31Sheria ya Mungu wake imo moyoni mwake; 2 nyayo zake hazitelezi. 1
32Watu waovu huvizia wenye haki, 2 wakitafuta kuwaua; 1
33lakini Bwana hatawaacha mikononi mwao 2 wala hatawaacha wahukumiwe 2 kuwa wakosa wanaposhtakiwa. 1
34Mngojee Bwana, 2 na uishike njia yake. 1 Naye atakutukuza uirithi nchi, 2 waovu watakapokatiliwa mbali, 2 utaliona hilo. 1
35Nimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi 2 kama mwerezi wa Lebanoni, 1
36lakini alitoweka mara na hakuonekana, 2 ingawa nilimtafuta, hakupatikana. 1
37Watafakari watu wasio na hatia, 2 wachunguze watu wakamilifu, 2 kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani. 1
38Lakini watenda dhambi wote wataangamizwa, 2 mafanikio yao yatakatiliwa mbali. 1
39Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Bwana, 2 yeye ni ngome yao wakati wa shida. 1
40Bwana huwasaidia na kuwaokoa, 2 huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi, 2 kwa maana wanamkimbilia.