Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 81

1Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu; 2 mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo! 1

2Anzeni wimbo, pigeni matari, 2 pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri. 1

3Pigeni baragumu za pembe za kondoo dume 2 wakati wa Mwandamo wa Mwezi, 1 na wakati wa mwezi mpevu, 2 katika siku ya Sikukuu yetu; 1

4hii ni amri kwa Israeli, 2 agizo la Mungu wa Yakobo. 1

5Aliiweka iwe kama sheria kwa Yosefu 2 alipotoka dhidi ya Misri, 2 huko tulikosikia lugha ambayo hatukuielewa. 1

6Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao; 2 mikono yao iliwekwa huru kutoka kwenye kikapu. 1

7Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa, 2 nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo; 2 nilikujaribu katika maji ya Meriba. 1

8“Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya: 2 laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli! 1

9Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu; 2 msimsujudie mungu wa kigeni. 1

10Mimi ni Bwana Mungu wako, 2 niliyekutoa nchi ya Misri. 1 Panua sana kinywa chako 2 nami nitakijaza. 1

11“Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza; 2 Israeli hakutaka kunitii. 1

12Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao 2 wafuate mashauri yao wenyewe. 1

13“Laiti kama watu wangu wangalinisikiliza, 2 kama Israeli wangalifuata njia zangu, 1

14ningaliwatiisha adui zao kwa haraka, 2 na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao! 1

15Wale wanaomchukia Bwana wangalinyenyekea mbele zake, 2 na adhabu yao ingedumu milele. 1

16Bali ninyi mngalilishwa ngano iliyo bora, 2 na kuwatosheleza kwa asali itokayo kwenye mwamba.”

← Psalms 80Read In The App, Free →Psalms 82 →

Study Psalms 81

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150