Psalms 142
1Namlilia Bwana kwa sauti, 2 nainua sauti yangu kwa Bwana anihurumie. 1
2Namimina malalamiko yangu mbele zake, 2 mbele zake naeleza shida zangu. 1
3Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu, 2 wewe ndiwe unajua njia zangu. 1 Katika njia ninayopita 2 watu wameniwekea mtego. 1
4Tazama kuume kwangu na uone, 2 hakuna hata mmoja anayejihusisha nami. 1 Sina kimbilio, 2 hakuna anayejali maisha yangu. 1
5Ee Bwana, nakulilia wewe, 2 nasema, “Wewe ni kimbilio langu, 2 fungu langu katika nchi ya walio hai.” 1
6Sikiliza kilio changu, 2 kwa sababu mimi ni mhitaji sana; 1 niokoe na wale wanaonifuatilia, 2 kwa kuwa wamenizidi nguvu. 1
7Nifungue kutoka kifungo changu, 2 ili niweze kulisifu jina lako. 1 Ndipo wenye haki watanizunguka, 2 kwa sababu ya wema wako kwangu.