Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 111

1Msifuni Bwana. 1 Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote, 2 katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko. 1

2Kazi za Bwana ni kuu, 2 wote wanaopendezwa nazo huzitafakari. 1

3Kazi zake zimejaa fahari na utukufu, 2 haki yake hudumu daima. 1

4Amefanya maajabu yake yakumbukwe, 2 Bwana ni mwenye neema na huruma. 1

5Huwapa chakula wale wanaomcha, 2 hulikumbuka agano lake milele. 1

6Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake, 2 akiwapa nchi za mataifa mengine. 1

7Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki, 2 mausia yake yote ni ya kuaminika. 1

8Zinadumu milele na milele, 2 zikifanyika kwa uaminifu na unyofu. 1

9Aliwapa watu wake ukombozi, 2 aliamuru agano lake milele: 2 jina lake ni takatifu na la kuogopwa. 1

10Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, 2 wote wanaozifuata amri zake wana busara. 2 Sifa zake zadumu milele.

← Psalms 110Read In The App, Free →Psalms 112 →

Study Psalms 111

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150