Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 85

1Ee Bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako. 2 Ulimrejeshea Yakobo baraka zake. + 85:1 Au: Uliwarudisha mateka wa Yakobo. 1

2Ulisamehe uovu wa watu wako, 2 na kufunika dhambi zao zote. 1

3Uliweka kando ghadhabu yako yote 2 na umegeuka na kuiacha hasira yako kali. 1

4Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena, 2 nawe uiondoe chuki yako juu yetu. 1

5Je, utatukasirikia milele? 2 Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote? 1

6Je, hutatuhuisha tena, 2 ili watu wako wakufurahie? 1

7Utuonyeshe upendo wako usiokoma, Ee Bwana, 2 utupe wokovu wako. 1

8Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana; 2 anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake: 2 lakini nao wasirudie upumbavu. 1

9Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao, 2 ili utukufu wake udumu katika nchi yetu. 1

10Upendo na uaminifu hukutana pamoja, 2 haki na amani hubusiana. 1

11Uaminifu huchipua kutoka nchi, 2 haki hutazama chini kutoka mbinguni. 1

12Naam, hakika Bwana atatoa kilicho chema, 2 nayo nchi yetu itazaa mavuno yake. 1

13Haki itatangulia mbele yake 2 na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake.

← Psalms 84Read In The App, Free →Psalms 86 →

Study Psalms 85

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150