Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 25

1Kwako wewe, Ee Bwana, 2 nainua nafsi yangu, 1

2ni wewe ninayekutumainia, 2 Ee Mungu wangu. 1 Usiniache niaibike, 2 wala usiache adui zangu wakanishinda. 1

3Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea 2 atakayeaibishwa, 1 bali wataaibishwa 2 wafanyao hila bila sababu. 1

4Nionyeshe njia zako, Ee Bwana, 2 nifundishe mapito yako, 1

5niongoze katika kweli yako na kunifundisha, 2 kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu, 2 nalo tumaini langu liko kwako wakati wote. 1

6Kumbuka, Ee Bwana, rehema zako kuu na upendo, 2 kwa maana zimekuwepo tangu zamani. 1

7Usizikumbuke dhambi za ujana wangu 2 wala njia zangu za uasi, 1 sawasawa na upendo wako unikumbuke, 2 kwa maana wewe ni mwema, Ee Bwana. 1

8Bwana ni mwema na mwenye adili, 2 kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake. 1

9Huwaongoza wanyenyekevu katika haki, 2 naye huwafundisha njia yake. 1

10Njia zote za Bwana ni za upendo na uaminifu 2 kwa wale wanaoshika shuhuda za agano lake. 1

11Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, 2 unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi. 1

12Ni nani basi, mtu yule anayemcha Bwana? 2 Atamfundisha katika njia 2 atakayoichagua kwa ajili yake. 1

13Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake, 2 nao wazao wake watairithi nchi. 1

14Siri ya Bwana iko kwa wale wamchao, 2 yeye huwajulisha agano lake. 1

15Macho yangu humwelekea Bwana daima, 2 kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa 2 miguu yangu kutoka mtego. 1

16Nigeukie na unihurumie, 2 kwa maana mimi ni mpweke na mwenye kuteseka. 1

17Shida za moyo wangu zimeongezeka, 2 niokoe katika dhiki yangu. 1

18Uangalie mateso na shida zangu 2 na uniondolee dhambi zangu zote. 1

19Tazama adui zangu walivyo wengi, 2 pia uone jinsi wanavyonichukia vikali! 1

20Uyalinde maisha yangu na uniokoe, 2 usiniache niaibike, 2 kwa maana nimekukimbilia wewe. 1

21Uadilifu na uaminifu vinilinde, 2 kwa sababu tumaini langu ni kwako. 1

22Ee Mungu, wakomboe Israeli, 2 katika shida zao zote!

← Psalms 24Read In The App, Free →Psalms 26 →

Study Psalms 25

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150