Psalms 145
1Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, 2 nitalisifu jina lako milele na milele. 1
2Kila siku nitakusifu 2 na kulitukuza jina lako milele na milele. 1
3Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, 2 ukuu wake haupimiki. 1
4Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, 2 watasimulia matendo yako makuu. 1
5Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, 2 nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu. 1
6Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, 2 nami nitatangaza matendo yako makuu. 1
7Wataadhimisha wema wako mwingi, 2 na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako. 1
8Bwana ni mwenye neema na mwingi wa huruma, 2 si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo. 1
9Bwana ni mwema kwa wote, 2 ana huruma kwa vyote alivyovifanya. 1
10Ee Bwana, vyote ulivyovifanya vitakusifu, 2 watakatifu wako watakutukuza. 1
11Watasimulia utukufu wa ufalme wako 2 na kusema juu ya ukuu wako, 1
12ili watu wote wajue matendo yako makuu 2 na utukufu wa fahari ya ufalme wako. 1
13Ufalme wako ni ufalme wa milele, 2 mamlaka yako hudumu vizazi vyote. 1 Bwana ni mwaminifu kwa ahadi zake zote 2 na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. 1
14Bwana huwategemeza wote waangukao, 2 na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao. 1
15Macho yao wote yanakutazama wewe, 2 nawe huwapa chakula chao wakati wake. 1
16Waufumbua mkono wako, 2 watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai. 1
17Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, 2 na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya. 1
18Bwana yu karibu na wote wamwitao, 2 karibu na wote wamwitao kwa uaminifu. 1
19Huwatimizia wamchao matakwa yao, 2 husikia kilio chao na kuwaokoa. 1
20Bwana huwalinda wote wampendao, 2 bali waovu wote atawaangamiza. 1
21Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana. 2 Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu 2 milele na milele.