Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 144

1Sifa ni kwa Bwana Mwamba wangu, 2 aifundishaye mikono yangu vita, 2 na vidole vyangu kupigana. 1

2Yeye ni Mungu wangu wa upendo na boma langu, 2 ngome yangu na mwokozi wangu, 1 ngao yangu ninayemkimbilia, 2 ambaye huwatiisha mataifa chini yangu. 1

3Ee Bwana, mwanadamu ni nini hata umjali, 2 Binadamu ni nini hata umfikirie? 1

4Mwanadamu ni kama pumzi, 2 siku zake ni kama kivuli kinachopita. 1

5Ee Bwana, pasua mbingu zako, ushuke, 2 gusa milima ili itoe moshi. 1

6Peleka umeme uwatawanye adui, 2 lenga mishale yako uwashinde. 1

7Nyoosha mkono wako kutoka juu, 2 nikomboe na kuniokoa 1 kutoka maji makuu, 2 kutoka mikononi mwa wageni 1

8ambao vinywa vyao vimejaa uongo, 2 na mikono yao ya kuume ni midanganyifu. 1

9Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, 2 kwa zeze yenye nyuzi kumi nitakuimbia, 1

10kwa Yule awapaye wafalme ushindi, 2 ambaye humwokoa Daudi, mtumishi wake kutokana na upanga hatari. 1

11Nikomboe na uniokoe 2 kutoka mikononi mwa wageni 1 ambao vinywa vyao vimejaa uongo, 2 na mikono yao ya kuume ni midanganyifu. 1

12Kisha wana wetu wakati wa ujana wao 2 watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri, 1 binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa 2 kurembesha jumba la kifalme. 1

13Ghala zetu zitajazwa 2 aina zote za mahitaji. 1 Kondoo zetu watazaa kwa maelfu, 2 kwa makumi ya maelfu katika mashamba yetu; 1

14maksai wetu watakokota 2 mizigo mizito. 1 Hakutakuwa na kubomoka kuta, 2 hakuna kuchukuliwa mateka, 1 wala kilio cha taabu 2 katika barabara zetu. 1

15Heri watu ambao hili ni kweli; 2 heri wale ambao Bwana ni Mungu wao.

← Psalms 143Read In The App, Free →Psalms 145 →

Study Psalms 144

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150