Psalms 45
1Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema 2 ninapomsimulia mfalme mabeti yangu; 2 ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi. 1
2Wewe ni bora kuliko watu wengine wote 2 na midomo yako imepakwa neema, 2 kwa kuwa Mungu amekubariki milele. 1
3Jifunge upanga wako pajani mwako, ee mwenye nguvu, 2 jivike fahari na utukufu. 1
4Katika fahari yako, songa mbele kwa ushindi, 2 kwa ajili ya kweli, unyenyekevu na haki, 2 mkono wako wa kuume na uonyeshe matendo ya kutisha. 1
5Mishale yako mikali na ichome mioyo ya adui za mfalme, 2 mataifa na yaanguke chini ya nyayo zako. 1
6Ee Mungu, kiti chako cha enzi 2 kitadumu milele na milele, 1 fimbo ya utawala wa haki 2 itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako. 1
7Unaipenda haki na kuchukia uovu; 2 kwa hiyo Mungu, Mungu wako, 1 amekuweka juu ya wenzako, 2 kwa kukupaka mafuta ya furaha. 1
8Mavazi yako yote yana harufu nzuri 2 ya manemane, udi na mdalasini; 1 kutoka kwenye majumba ya kifalme 2 yaliyopambwa kwa pembe za ndovu, 1 sauti za vinanda vya nyuzi 2 zinakufanya ufurahi. 1
9Binti za wafalme ni miongoni mwa wanawake wako waheshimiwa; 2 kuume kwako yupo bibi arusi malkia aliyevaa dhahabu ya Ofiri. 1
10Sikiliza, ewe binti, fikiri na utege sikio: 2 Sahau watu wako na nyumba ya baba yako. 1
11Mfalme ameshangazwa na uzuri wako; 2 mheshimu, kwa kuwa yeye ni bwana wako. 1
12Binti wa Tiro atakuletea zawadi, 2 watu wenye utajiri watatafuta upendeleo wako. 1
13Utukufu wote una binti mfalme katika chumba chake; 2 vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu. 1
14Anaongozwa kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi yaliyotariziwa, 2 mabikira wenzake wanamfuata 2 na wanaletwa kwako. 1
15Wanaingizwa ndani kwa shangwe na furaha, 2 na kuingia katika jumba la mfalme. 1
16Wana wenu watachukua nafasi za baba zenu, 2 mtawafanya wakuu katika nchi yote. 1
17Nitadumisha kumbukumbu lako katika vizazi vyote, 2 kwa hiyo mataifa watakusifu milele na milele.