Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 77

1Nilimlilia Mungu ili anisaidie, 2 nilimlilia Mungu ili anisikie. 1

2Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana, 2 usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka 2 na nafsi yangu ilikataa kufarijika. 1

3Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nikalia kwa huzuni; 2 nikatafakari, roho yangu ikadhoofika. 1

4Ulizuia macho yangu kufumba; 2 nilikuwa nasumbuka, nikashindwa kusema. 1

5Nilitafakari juu ya siku zilizopita, 2 miaka mingi iliyopita, 1

6nilikumbuka nilivyoimba nyimbo usiku. 2 Moyo wangu ulitafakari 2 na roho yangu ikauliza: 1

7“Je, Bwana atakataa milele? 2 Je, hatatenda mema tena? 1

8Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele? 2 Je, ahadi yake imekoma nyakati zote? 1

9Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? 2 Je, katika hasira amezuia huruma yake?” 1

10Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: 2 lakini nitakumbuka 1 miaka ya mkono wa kuume 2 wa Aliye Juu Sana.” 1

11Nitayakumbuka matendo ya Bwana; 2 naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani. 1

12Nitazitafakari kazi zako zote 2 na kuyawaza matendo yako makuu. 1

13Ee Mungu, njia zako ni takatifu. 1 Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu? 1

14Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, 2 umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa. 1

15Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako, 2 uzao wa Yakobo na Yosefu. 1

16Maji yalikuona, Ee Mungu, 2 maji yalikuona yakakimbia, 2 vilindi vilitetemeka. 1

17Mawingu yalimwaga maji, 2 mbingu zikatoa ngurumo kwa radi, 2 mishale yako ikametameta huku na huko. 1

18Ngurumo yako ilisikika katika upepo wa kisulisuli, 2 umeme wako wa radi ukaangaza dunia, 2 nchi ikatetemeka na kutikisika. 1

19Njia yako ilipita baharini, 2 mapito yako kwenye maji makuu, 2 ingawa nyayo zako hazikuonekana. 1

20Uliongoza watu wako kama kundi 2 kwa mkono wa Mose na Aroni.

← Psalms 76Read In The App, Free →Psalms 78 →

Study Psalms 77

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150