Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 137

1Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza 2 tulipokumbuka Sayuni. 1

2Kwenye miti ya huko 2 tulitundika vinubi vyetu, 1

3kwa maana huko hao waliotuteka 2 walitaka tuwaimbie nyimbo, 1 watesi wetu walidai nyimbo za furaha; 2 walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!” 1

4Tutaimbaje nyimbo za Bwana, 2 tukiwa nchi ya kigeni? 1

5Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu, 2 basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake. 1

6Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changu 2 kama sitakukumbuka wewe, 1 kama nisipokufikiri Yerusalemu 2 kuwa furaha yangu kubwa. 1

7Kumbuka, Ee Bwana, walichokifanya Waedomu, 2 siku ile Yerusalemu ilipoanguka. 1 Walisema, “Bomoa, Bomoa 2 mpaka kwenye misingi yake!” 1

8Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa, 2 heri yeye atakayekulipiza wewe 2 kwa yale uliyotutenda sisi: 1

9yeye ambaye atawakamata watoto wako wachanga 2 na kuwaponda juu ya miamba.

← Psalms 136Read In The App, Free →Psalms 138 →

Study Psalms 137

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150