Psalms 74
1Ee Mungu, mbona umetukataa milele? 2 Mbona hasira yako inatoka moshi 2 juu ya kondoo wa malisho yako? 1
2Kumbuka watu uliowanunua zamani, 2 kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa: 2 Mlima Sayuni, ambamo uliishi. 1
3Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu, 2 uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu. 1
4Adui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi, 2 wanaweka bendera zao kama alama. 1
5Walifanya kama watu wanaotumia mashoka 2 kukata kichaka cha miti. 1
6Walivunjavunja milango yote iliyonakshiwa 2 kwa mashoka na vishoka vyao. 1
7Waliteketeza kabisa mahali pako patakatifu, 2 wakayanajisi makao ya Jina lako. 1
8Walisema mioyoni mwao, 2 “Tutawaponda kabisa!” 1 Walichoma kila mahali ambapo Mungu 2 aliabudiwa katika nchi. 1
9Hatukupewa ishara za miujiza; 2 hakuna manabii waliobaki, 1 hakuna yeyote kati yetu ajuaye 2 hali hii itachukua muda gani. 1
10Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini? 2 Je, adui watalitukana jina lako milele? 1
11Kwa nini unazuia mkono wako, 2 mkono wako wa kuume? 1 Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako 2 na uwaangamize! 1
12Lakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani, 2 unaleta wokovu duniani. 1
13Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako; 2 ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji. 1
14Ni wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani + 74:14 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. 2 nawe ukamtoa kama chakula 2 kwa viumbe vya jangwani. 1
15Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito, 2 ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima. 1
16Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia, 2 uliziweka jua na mwezi. 1
17Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia, 2 ulifanya kiangazi na masika. 1
18Ee Bwana, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki, 2 jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako. 1
19Usiukabidhi uhai wa njiwa wako kwa wanyama wakali wa mwitu; 2 usisahau kabisa uhai wa watu wako wanaoteseka milele. 1
20Likumbuke agano lako, 2 maana mara kwa mara mambo ya jeuri 2 yamejaa katika sehemu za giza nchini. 1
21Usiruhusu walioonewa warudi nyuma kwa aibu; 2 maskini na wahitaji hebu walisifu jina lako. 1
22Inuka, Ee Mungu, ujitetee; 2 kumbuka jinsi wapumbavu 2 wanavyokudhihaki mchana kutwa. 1
23Usipuuze makelele ya watesi wako, 2 ghasia za adui zako, zinazoinuka mfululizo.