Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 141

1Ee Bwana, ninakuita wewe, uje kwangu hima. 2 Sikia sauti yangu ninapokuita. 1

2Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba; 2 kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni. 1

3Ee Bwana, weka mlinzi kinywani mwangu, 2 weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu. 1

4Usiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya, 2 nisije nikashiriki katika matendo maovu 1 pamoja na watu watendao mabaya, 2 wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa. 1

5Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma; 2 na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu. 2 Kichwa changu hakitalikataa. 1 Hata hivyo, maombi yangu daima 2 ni kinyume cha watenda mabaya, 1

6watawala wao watatupwa chini 2 kutoka kwenye majabali, 1 waovu watajifunza kwamba maneno yangu 2 yalikuwa kweli. 1

7Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi, 2 ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.” 1

8Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mwenyezi, 2 ndani yako nimekimbilia, usiniache nife. 1

9Niepushe na mitego waliyonitegea, 2 kutokana na mitego iliyotegwa na watenda mabaya. 1

10Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe, 2 wakati mimi ninapita salama.

← Psalms 140Read In The App, Free →Psalms 142 →

Study Psalms 141

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150