Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 46

1Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, 2 msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. 1

2Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa 2 nayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari. 1

3Hata kama maji yake yatanguruma na kuumuka, 2 milima nayo ikitetemeka kwa mawimbi yake. 1

4Kuna mto ambao vijito vyake vinaufurahisha mji wa Mungu, 2 mahali patakatifu ambako Aliye Juu Sana anaishi. 1

5Mungu yuko katikati yake, hautaanguka, 2 Mungu atausaidia asubuhi na mapema. 1

6Mataifa yanafanya ghasia, falme zinaanguka, 2 Yeye huinua sauti yake, dunia ikayeyuka. 1

7Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi, 2 Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. 1

8Njooni mkaone kazi za Bwana 2 jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi. 1

9Anakomesha vita hata miisho ya dunia, 2 anakata upinde na kuvunjavunja mkuki, 2 anateketeza ngao kwa moto. 1

10“Tulieni, mjue ya kwamba mimi ndimi Mungu; 2 nitatukuzwa katikati ya mataifa, 2 nitatukuzwa katika dunia.” 1

11Bwana Mwenye Nguvu Zote yu pamoja nasi; 2 Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.

← Psalms 45Read In The App, Free →Psalms 47 →

Study Psalms 46

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150