Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 80

1Ee Mchungaji wa Israeli tusikie, 2 wewe umwongozaye Yosefu kama kundi; 1 wewe uketiye katika kiti cha enzi 2 katikati ya makerubi, angaza 2

2mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase. 1 Uamshe nguvu zako, 2 uje utuokoe. 1

3Ee Mungu, uturejeshe, 2 utuangazie uso wako, 2 ili tuweze kuokolewa. 1

4Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, 2 hata lini hasira yako itawaka na kufoka moshi 2 dhidi ya maombi ya watu wako? 1

5Umewalisha kwa mkate wa machozi, 2 umewafanya wanywe machozi bakuli tele. 1

6Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu, 2 na adui zetu wanatudhihaki. 1

7Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; 2 utuangazie uso wako, 2 nasi tuweze kuokolewa. 1

8Ulileta mzabibu kutoka Misri, 2 ukawafukuza mataifa, ukaupanda. 1

9Uliandaa shamba kwa ajili yake, 2 mizizi ikawa imara, ukajaza nchi. 1

10Milima ilifunikwa kwa kivuli chake, 2 matawi yake yakafunika mierezi mikubwa. 1

11Matawi yake yalienea mpaka Baharini, + 80:11 Huenda inamaanisha Bahari ya Mediterania. 2 machipukizi yake mpaka kwenye Mto. + 80:11 Yaani Mto Frati. 1

12Mbona umebomoa kuta zake 2 ili wote wapitao karibu 2 wazichume zabibu zake? 1

13Nguruwe mwitu wanauharibu 2 na wanyama wa kondeni hujilisha humo. 1

14Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote! 2 Tazama chini kutoka mbinguni na uone! 1 Linda mzabibu huu, 2

15mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume, 1 mwana uliyemlea 2 kwa ajili yako mwenyewe. 1

16Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto, 2 unapowakemea, watu wako huangamia. 1

17Mkono wako na utulie juu ya mtu aliyeko mkono wako wa kuume, 2 mwana wa mtu uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe. 1

18Ndipo hatutakuacha tena, 2 utuhuishe, nasi tutaliitia jina lako. 1

19Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; 2 utuangazie uso wako, 2 ili tuweze kuokolewa.

← Psalms 79Read In The App, Free →Psalms 81 →

Study Psalms 80

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150