Psalms 102
1Ee Bwana, usikie maombi yangu, 2 kilio changu cha kuomba msaada kikufikie. 1
2Usinifiche uso wako 2 ninapokuwa katika shida. 1 Unitegee sikio lako, 2 ninapoita, unijibu kwa upesi. 1
3Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi, 2 mifupa yangu inaungua kama kaa la moto. 1
4Moyo wangu umefifia na kunyauka kama jani, 2 ninasahau kula chakula changu. 1
5Kwa sababu ya kusononeka kwangu kwa uchungu, 2 nimebakia ngozi na mifupa. 1
6Nimekuwa kama bundi wa jangwani, 2 kama bundi kwenye magofu. 1
7Nilalapo sipati usingizi, 2 nimekuwa kama ndege mpweke 2 kwenye paa la nyumba. 1
8Mchana kutwa adui zangu hunidhihaki, 2 wale wanaonizunguka hutumia jina langu kama laana. 1
9Ninakula majivu kama chakula changu 2 na nimechanganya kinywaji changu na machozi 1
10kwa sababu ya ghadhabu yako kuu, 2 kwa maana umeniinua na kunitupa kando. 1
11Siku zangu ni kama kivuli cha jioni, 2 ninanyauka kama jani. 1
12Lakini wewe, Ee Bwana, umeketi katika kiti chako cha enzi milele, 2 sifa zako za ukuu zaendelea vizazi vyote. 1
13Utainuka na kuihurumia Sayuni, 2 kwa maana ni wakati wa kumwonyesha wema; 2 wakati uliokubalika umewadia. 1
14Kwa maana mawe yake ni ya thamani kwa watumishi wako, 2 vumbi lake lenyewe hulionea huruma. 1
15Mataifa wataogopa jina la Bwana, 2 wafalme wote wa dunia watauheshimu utukufu wako. 1
16Kwa maana Bwana ataijenga tena Sayuni 2 na kutokea katika utukufu wake. 1
17Ataitikia maombi ya mtu mkiwa, 2 wala hatadharau hoja yao. 1
18Hili na liandikwe kwa ajili ya kizazi kijacho, 2 ili taifa litakaloumbwa baadaye waweze kumsifu Bwana: 1
19“ Bwana alitazama chini kutoka patakatifu pake palipo juu, 2 kutoka mbinguni alitazama dunia, 1
20kusikiliza vilio vya uchungu vya wafungwa 2 na kuwaweka huru wale waliohukumiwa kufa.” 1
21Kwa hiyo jina la Bwana latangazwa huko Sayuni 2 na sifa zake katika Yerusalemu, 1
22wakati mataifa na falme zitakapokusanyika 2 ili kumwabudu Bwana. 1
23Katika kuishi kwangu alivunja nguvu zangu, 2 akafupisha siku zangu. 1
24Ndipo niliposema: 2 “Ee Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu; 2 miaka yako inaendelea vizazi vyote. 1
25Hapo mwanzo uliweka misingi ya dunia, 2 nazo mbingu ni kazi ya mikono yako. 1
26Hizi zitatoweka, lakini wewe utadumu, 2 zote zitachakaa kama vazi. 1 Utazibadilisha kama nguo 2 nazo zitaondoshwa. 1
27Lakini wewe, U yeye yule, 2 nayo miaka yako haikomi kamwe. 1
28Watoto wa watumishi wako wataishi mbele zako; 2 wazao wao wataimarishwa mbele zako.”