Psalms 115
1Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi, 2 bali utukufu ni kwa jina lako, 1 kwa sababu ya upendo 2 na uaminifu wako. 1
2Kwa nini mataifa waseme, 2 “Yuko wapi Mungu wao?” 1
3Mungu wetu yuko mbinguni, 2 naye hufanya lolote limpendezalo. 1
4Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu, 2 zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. 1
5Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, 2 zina macho, lakini haziwezi kuona; 1
6zina masikio, lakini haziwezi kusikia, 2 zina pua, lakini haziwezi kunusa; 1
7zina mikono, lakini haziwezi kupapasa, 2 zina miguu, lakini haziwezi kutembea; 2 wala koo zao haziwezi kutoa sauti. 1
8Wale wanaozitengeneza watafanana nazo, 2 vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia. 1
9Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Bwana, 2 yeye ni msaada na ngao yao. 1
10Ee nyumba ya Aroni, mtumainini Bwana, 2 yeye ni msaada na ngao yao. 1
11Ninyi mnaomcha, mtumainini Bwana, 2 yeye ni msaada na ngao yao. 1
12Bwana anatukumbuka na atatubariki: 2 ataibariki nyumba ya Israeli, 2 ataibariki nyumba ya Aroni, 1
13atawabariki wale wanaomcha Bwana, 2 wadogo kwa wakubwa. 1
14Bwana na awawezeshe kuongezeka, 2 ninyi na watoto wenu. 1
15Mbarikiwe na Bwana 2 Muumba wa mbingu na dunia. 1
16Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Bwana, 2 lakini dunia amempa mwanadamu. 1
17Sio wafu wanaomsifu Bwana, 2 wale washukao mahali pa kimya, + 115:17 Mahali pa kimya maana yake ni Kuzimu, yaani Sheol kwa Kiebrania. 1
18bali ni sisi tunaomtukuza Bwana, 2 sasa na hata milele. 1 Msifuni Bwana. + 115:18 Msifuni Bwana ni Kiebrania Hallelu Yah.