Psalms 94
1Ee Bwana, ulipizaye kisasi, 2 Ee Mungu ulipizaye kisasi, uangaze sasa. 1
2Ee Mhukumu wa dunia, inuka, 2 uwalipize wenye kiburi kama wanavyostahili. 1
3Hata lini, waovu, Ee Bwana, 2 hata lini waovu watashangilia? 1
4Wanamimina maneno ya kiburi, 2 watenda mabaya wote wamejaa majivuno. 1
5Ee Bwana, wanawaponda watu wako, 2 wanawaonea urithi wako. 1
6Wanamchinja mjane na mgeni, 2 na kuwaua yatima. 1
7Nao husema, “ Bwana haoni, 2 Mungu wa Yakobo hafahamu.” 1
8Sikizeni, enyi wajinga miongoni mwa watu; 2 enyi wapumbavu, lini mtakuwa na hekima? 1
9Je, aliyeweka sikio asisikie? 2 Aliyeumba jicho asione? 1
10Je, anayeadhibisha mataifa asiadhibu? 2 Je, awafundishaye wanadamu asiwe na maarifa? 1
11Bwana anajua mawazo ya mwanadamu; 2 anajua kwamba ni ubatili. 1
12Ee Bwana, heri mtu anayeadhibishwa na wewe, 2 mtu unayemfundisha kwa sheria yako, 1
13unampa utulivu siku za shida, 2 mpaka shimo litakapokuwa limechimbwa 2 kwa ajili ya mwovu. 1
14Kwa kuwa Bwana hatawakataa watu wake, 2 hatauacha urithi wake. 1
15Hukumu itasimamishwa tena kwenye haki, 2 wote walio na mioyo minyofu wataifuata. 1
16Ni nani atakayeinuka dhidi ya mwovu kwa ajili yangu? 2 Ni nani atakayenikinga dhidi ya watenda maovu? 1
17Kama Bwana asingelinisaidia upesi, 2 ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo. 1
18Niliposema, “Mguu wangu unateleza,” 2 Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia. 1
19Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu, 2 faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu. 1
20Je, kiti cha utawala wa udhalimu kitajiunga nawe, 2 ule utawala uletao taabu kutokana na sheria zake? 1
21Huungana kuwashambulia wenye haki, 2 kuwahukumu kufa wasio na hatia. 1
22Lakini Bwana amekuwa ngome yangu, 2 na Mungu wangu amekuwa mwamba ninaoukimbilia. 1
23Yeye atawalipa kwa ajili ya dhambi zao 2 na atawaangamiza kwa ajili ya maovu yao; 2 Bwana Mungu wetu atawaangamiza.