Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 136

1Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele. 1

2Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele. 1

3Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele. 1

4Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele. 1

5Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele. 1

6Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele. 1

7Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele. 1

8Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele. 1

9Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele. 1

10Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, Fadhili zake zadumu milele. 1

11Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele. 1

12Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, Fadhili zake zadumu milele. 1

13Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele. 1

14Na kuwapitisha Israeli katikati yake, Fadhili zake zadumu milele. 1

15Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele. 1

16Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa, Fadhili zake zadumu milele. 1

17Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele. 1

18Naye aliwaua wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele. 1

19Sihoni mfalme wa Waamori, Fadhili zake zadumu milele. 1

20Ogu mfalme wa Bashani, Fadhili zake zadumu milele. 1

21Akatoa nchi yao kuwa urithi, Fadhili zake zadumu milele. 1

22Urithi kwa Israeli mtumishi wake, Fadhili zake zadumu milele. 1

23Aliyetukumbuka katika unyonge wetu, Fadhili zake zadumu milele. 1

24Alituweka huru toka adui zetu, Fadhili zake zadumu milele. 1

25Ambaye humpa chakula kila kiumbe. Fadhili zake zadumu milele. 1

26Mshukuruni Mungu wa mbinguni, Fadhili zake zadumu milele.

← Psalms 135Read In The App, Free →Psalms 137 →

Study Psalms 136

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150