Psalms 86
1Ee Bwana, sikia na unijibu, 2 kwa maana mimi ni maskini na mhitaji. 1
2Linda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako, 2 wewe ni Mungu wangu, 2 mwokoe mtumishi wako anayekutumaini. 1
3Ee Bwana, nihurumie mimi, 2 kwa maana ninakuita mchana kutwa. 1
4Mpe mtumishi wako furaha, 2 kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana, 2 ninainua nafsi yangu. 1
5Ee Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe, 2 umejaa upendo kwa wote wakuitao. 1
6Ee Bwana, sikia maombi yangu, 2 sikiliza kilio changu unihurumie. 1
7Katika siku ya shida yangu nitakuita, 2 kwa maana wewe utanijibu. 1
8Ee Bwana, katikati ya miungu hakuna kama wewe, 2 hakuna matendo ya kulinganishwa na yako. 1
9Ee Bwana, mataifa yote uliyoyafanya 2 yatakuja na kuabudu mbele zako; 2 wataliletea utukufu jina lako. 1
10Kwa maana wewe ni mkuu, na unafanya mambo ya ajabu; 2 wewe peke yako ndiwe Mungu. 1
11Ee Bwana, nifundishe njia yako, 2 nami nitakwenda katika kweli yako; 1 nipe moyo usiositasita, 2 ili niweze kulicha jina lako. 1
12Ee Bwana wangu, nitakusifu kwa moyo wote; 2 nitaliadhimisha jina lako milele. 1
13Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu; 2 umeniokoa kutoka kwenye vilindi vya kaburi. + 86:13 Yaani Kuzimu. 1
14Ee Mungu, wenye majivuno wananishambulia; 2 kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu: 2 watu wasiokuheshimu wewe. 1
15Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema, 2 si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu. 1
16Nigeukie na unihurumie; 2 mpe mtumishi wako nguvu zako, 2 mwokoe mwana wa mtumishi wako wa kike. + 86:16 Au: mwokoe mwanao mwaminifu. 1
17Nipe ishara ya wema wako, 2 ili adui zangu waione nao waaibishwe, 1 kwa kuwa wewe, Ee Bwana, 2 umenisaidia na kunifariji.