Psalms 84
1Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 makao yako yapendeza kama nini! 1
2Nafsi yangu inatamani sana, 2 naam, hata kuona shauku, 2 kwa ajili ya nyua za Bwana; 1 moyo wangu na mwili wangu 2 vinamlilia Mungu Aliye Hai. 1
3Hata shomoro amejipatia makao, 2 mbayuwayu amejipatia kiota 2 mahali awezapo kuweka makinda yake: 1 mahali karibu na madhabahu yako, 2 Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 Mfalme wangu na Mungu wangu. 1
4Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, 2 wanaokusifu wewe daima. 1
5Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako, 2 na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao. 1
6Wanapopita katika Bonde la Baka, + 84:6 Yaani Bonde la Vilio. 2 hulifanya mahali pa chemchemi, 2 pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi. + 84:6 Au: baraka. 1
7Huendelea toka nguvu hadi nguvu, 2 hadi kila mmoja afikapo 2 mbele za Mungu huko Sayuni. 1
8Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, sikia maombi yangu; 2 nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo. 1
9Ee Mungu, uitazame ngao yetu, 2 mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako. 1
10Siku moja katika nyua zako ni bora 2 kuliko siku elfu mahali pengine; 1 afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu 2 kuliko kukaa katika mahema ya waovu. 1
11Kwa kuwa Bwana ni jua na ngao, 2 Bwana hutoa wema na heshima; 1 hakuna kitu chema anachowanyima 2 wale ambao hawana hatia. 1
12Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.