Psalms 88
1Ee Bwana, Mungu uniokoaye, 2 nimelia mbele zako usiku na mchana. 1
2Maombi yangu yafike mbele zako, 2 utegee kilio changu sikio lako. 1
3Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu, 2 na maisha yangu yanakaribia kaburi. + 88:3 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. 1
4Nimehesabiwa miongoni mwa wale waendao shimoni, 2 niko kama mtu asiye na nguvu. 1
5Nimetengwa pamoja na wafu, 2 kama waliochinjwa walalao kaburini, 1 ambao huwakumbuki tena, 2 ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako. 1
6Umenitupa katika shimo lenye kina kirefu sana, 2 katika vina vya giza nene. 1
7Ghadhabu yako imekuwa nzito juu yangu, 2 umenigharikisha kwa mawimbi yako yote. 1
8Umenitenga na rafiki zangu wa karibu 2 na kunifanya chukizo kwao. 1 Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka; 2
9nuru ya macho yangu 2 imefifia kwa ajili ya huzuni. 1 Ee Bwana, ninakuita kila siku, 2 ninakunyooshea wewe mikono yangu. 1
10Je, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako? 2 Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu? 1
11Je, upendo wako hutangazwa kaburini, 2 uaminifu wako katika Uharibifu? + 88:11 Yaani Abadon . 1
12Je, maajabu yako hujulikana mahali pa giza, 2 au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu? 1
13Lakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie; 2 asubuhi maombi yangu huja mbele zako. 1
14Ee Bwana, kwa nini unanikataa 2 na kunificha uso wako? 1
15Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo; 2 nimepatwa na hofu zako, nami nimekata tamaa. 1
16Ghadhabu yako imepita juu yangu; 2 hofu zako zimeniangamiza. 1
17Mchana kutwa zinanizunguka kama mafuriko; 2 zimenimeza kabisa. 1
18Umeniondolea marafiki na wapendwa wangu; 2 giza limekuwa ndilo rafiki yangu wa karibu kuliko wote.