Psalms 6
1Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, 2 wala usiniadhibu katika ghadhabu yako. 1
2Unirehemu Bwana, 2 kwa maana nimedhoofika; 1 Ee Bwana, uniponye, 2 kwa maana mifupa yangu 2 ina maumivu makali. 1
3Nafsi yangu ina uchungu mwingi. 2 Mpaka lini, Ee Bwana, mpaka lini? 1
4Geuka Ee Bwana, unikomboe, 2 uniokoe kwa sababu ya fadhili zako. 1
5Hakuna mtu anayekukumbuka 2 akiwa amekufa. 1 Ni nani awezaye kukusifu 2 akiwa kuzimu? 1
6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni; 2 usiku kucha nafurikisha 2 kitanda changu kwa machozi; 1 nimelowesha viti vyangu vya fahari 2 kwa machozi. 1
7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika, 2 yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote. 1
8Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya, 2 kwa maana Bwana amesikia kulia kwangu. 1
9Bwana amesikia kilio changu kwa huruma, 2 Bwana amekubali sala yangu. 1
10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika, 2 watarudi nyuma kwa aibu ya ghafula.