Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 9

1Ee Bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote, 2 nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu. 1

2Nitafurahi na kushangilia ndani yako. 2 Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana. 1

3Adui zangu wamerudi nyuma, 2 wamejikwaa na kuangamia mbele zako. 1

4Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu; 2 umeketi kwenye kiti chako cha enzi, 2 ukihukumu kwa haki. 1

5Umekemea mataifa na kuwaangamiza waovu; 2 umeyafuta majina yao milele na milele. 1

6Uharibifu usiokoma umempata adui, 2 umeingʼoa miji yao; 2 hata kumbukumbu lao limetoweka. 1

7Bwana anatawala milele, 2 ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu. 1

8Mungu atahukumu ulimwengu kwa haki, 2 atatawala mataifa kwa haki. 1

9Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa, 2 ni ngome imara wakati wa shida. 1

10Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe, 2 kwa maana wewe Bwana, 2 hujawaacha kamwe wakutafutao. 1

11Mwimbieni Bwana sifa, amefanywa mtawala Sayuni, 2 tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda. 1

12Kwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka, 2 hapuuzi kilio cha wanaoonewa. 1

13Ee Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa! 2 Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti, 1

14ili niweze kutangaza sifa zako 2 katika malango ya Binti Sayuni 2 na huko niushangilie wokovu wako. 1

15Mataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba, 2 miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha. 1

16Bwana anajulikana kwa haki yake, 2 waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao. 1

17Waovu wataishia kuzimu, 2 naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. 1

18Lakini mhitaji hatasahaulika siku zote, 2 wala matumaini ya walioonewa hayatapotea. 1

19Ee Bwana, inuka, usimwache binadamu ashinde. 2 Mataifa na yahukumiwe mbele zako. 1

20Ee Bwana, wapige kwa hofu, 2 mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.

← Psalms 8Read In The App, Free →Psalms 10 →

Study Psalms 9

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150