Psalms 41
1Heri mtu yule anayemjali mnyonge, 2 Bwana atamwokoa wakati wa shida. 1
2Bwana atamlinda na kuyahifadhi maisha yake, 2 atambariki katika nchi 2 na hatamwacha katika tamaa ya adui zake. 1
3Bwana atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani, 2 atamwinua kutoka kitandani mwake. 1
4Nilisema, “Ee Bwana nihurumie, 2 niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.” 1
5Adui zangu wanasema kwa hila, 2 “Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.” 1
6Kila anapokuja mtu kunitazama, 2 huzungumza uongo, 1 huku moyo wake hukusanya masingizio; 2 kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko. 1
7Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu, 2 hao huniwazia mabaya sana, wakisema, 1
8“Ugonjwa mbaya sana umempata, 2 kamwe hatainuka tena kitandani mwake.” 1
9Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini, 2 yule aliyekula chakula changu 2 ameniinulia kisigino chake. 1
10Lakini wewe, Ee Bwana, nihurumie, 2 ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi. 1
11Najua kwamba wapendezwa nami, 2 kwa kuwa adui yangu hanishindi. 1
12Katika uadilifu wangu unanitegemeza 2 na kuniweka kwenye uwepo wako milele. 1
13Msifuni Bwana, Mungu wa Israeli, 2 tangu milele na hata milele. Amen na Amen.