Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 58

1Enyi watawala, je, kweli mwanena kwa haki? 2 Je, mnahukumu kwa unyofu miongoni mwa watu? 1

2La, mioyoni mwenu mnatunga udhalimu, 2 na mikono yenu hupima jeuri duniani. 1

3Waovu ni wapotovu tangu kuzaliwa kwao, 2 toka tumboni mwa mama zao 2 ni wakaidi na husema uongo. 1

4Sumu yao ni kama sumu ya nyoka, 2 kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake, 1

5ambaye hatasikia sauti ya kutumbuiza ya mwaguzi, 2 hata kama mganga angecheza kwa ustadi kiasi gani. 1

6Ee Mungu, yavunje meno katika vinywa vyao; 2 Ee Bwana, vunja meno makali ya hao simba! 1

7Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi, 2 wavutapo pinde zao, mishale yao na iwe butu. 1

8Kama konokono ayeyukavyo akitembea, 2 kama mtoto aliyezaliwa akiwa mfu, 2 wasilione jua. 1

9Kabla vyungu vyenu havijapata moto wa kuni za miiba, 2 zikiwa mbichi au kavu, 1 waovu watakuwa 2 wamefagiliwa mbali. 1

10Wenye haki watafurahi waonapo wakilipizwa kisasi, 2 watakapochovya nyayo zao katika damu ya waovu. 1

11Ndipo wanadamu watasema, 2 “Hakika utulivu wa wenye haki bado una thawabu, 2 hakika kuna Mungu ahukumuye dunia.”

← Psalms 57Read In The App, Free →Psalms 59 →

Study Psalms 58

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150