Psalms 8
1Ee Bwana, Bwana wetu, 2 tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! 1 Umeuweka utukufu wako 2 juu ya mbingu. 1
2Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao 2 umeamuru sifa, 1 kwa sababu ya watesi wako, 2 kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi. 1
3Nikiziangalia mbingu zako, 2 kazi ya vidole vyako, 1 mwezi na nyota, 2 ulizoziratibisha, 1
4mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, 2 binadamu ni nani hata unamjali? 1
5Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, 2 ukamvika taji ya utukufu na heshima. 1
6Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako; 2 umeweka vitu vyote chini ya miguu yake. 1
7Mifugo na makundi yote pia, 2 naam, na wanyama wa kondeni, 1
8ndege wa angani na samaki wa baharini, 2 naam, kila kiogeleacho katika njia za bahari. 1
9Ee Bwana, Bwana wetu, 2 tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!