Psalms 112
1Msifuni Bwana. 1 Heri mtu yule amchaye Bwana, 2 mtu yule apendezwaye sana na amri zake. 1
2Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi, 2 kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa. 1
3Nyumbani mwake kuna mali na utajiri, 2 haki yake hudumu milele. 1
4Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu, 2 yule mwenye rehema, huruma na haki. 1
5Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba, 2 anayefanya mambo yake kwa haki. 1
6Hakika hatatikisika kamwe, 2 mtu mwenye haki atakumbukwa milele. 1
7Hataogopa habari mbaya, 2 moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana. 1
8Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu, 2 mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake. 1
9Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini; 2 haki yake hudumu milele; 2 pembe yake itatukuzwa kwa heshima. 1
10Mtu mwovu ataona na kuchukizwa, 2 atasaga meno yake na kutoweka, 2 kutamani kwa mtu mwovu kutaishia patupu.