Psalms · Biblia (Kiswahili)

Psalms 96

1Mwimbieni Bwana wimbo mpya; 2 mwimbieni Bwana dunia yote. 1

2Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake; 2 tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. 1

3Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, 2 matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. 1

4Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; 2 yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. 1

5Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, 2 lakini Bwana aliziumba mbingu. 1

6Fahari na enzi viko mbele yake; 2 nguvu na utukufu vimo patakatifu pake. 1

7Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, 2 mpeni Bwana utukufu na nguvu. 1

8Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; 2 leteni sadaka na mje katika nyua zake. 1

9Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake; 2 dunia yote na itetemeke mbele zake. 1

10Katikati ya mataifa semeni, “ Bwana anatawala.” 1 Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa; 2 atawahukumu watu kwa uadilifu. 1

11Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; 2 bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; 1

12mashamba na yashangilie, 2 pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. 1 Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha; 2

13itaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja, 2 anakuja kuihukumu dunia. 1 Ataihukumu dunia kwa haki, 2 na mataifa katika kweli yake.

← Psalms 95Read In The App, Free →Psalms 97 →

Study Psalms 96

KJVMatthew HenryJamieson-Fausset-BrownAdam ClarkeJohn WesleyJohn CalvinKeil and DelitzschCharles SpurgeonScofieldFamily Bible NotesGeneva Bible Notes (1599)Reina-Valera (Español)Bíblia Almeida (Português)Luther Bibel (Deutsch)Bible Louis Segond (Français)

All Chapters

123456789101112131415161718192021222324252627282930313233343536373839404142434445464748495051525354555657585960616263646566676869707172737475767778798081828384858687888990919293949596979899100101102103104105106107108109110111112113114115116117118119120121122123124125126127128129130131132133134135136137138139140141142143144145146147148149150